Chama Aongeza Mkataba Mpya Simba SC

NancyTheDreamtz

MFUNGAJI wa mabao ya mwisho yaliyoipeleka hatua ya makundi na Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika timu ya Simba Mzambia, Clatous Chota Chama ‘Triple C’ ameongeza mkataba mwingine wa miaka miwili
ya kuendelea kuichezea timu hiyo.
Huyo, ni mchezaji wa sita kwa Simba kuongezewa mkataba wengine ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Aishi Manula, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Meddie Kagere. Chama alijiunga na Simba kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akitokea Power Dynamo inayocheza ligi ya nchini huko.

Taarifa ya klabu ya Simba inaeleza kuwa kiungo huyo atakuwa sehemu ya kikosi hicho hadi 2020 baada ya kuongeza mkataba huo. Simba hivi sasa ipo kwenye mikakati ya kukiboresha kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kimataifa Afrika na kikubwa kufika hatua ya fainali baada ya msimu uliopita kufika robo fainali.

Timu hiyo hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kuwasajili wachezaji wapya watano ambao ni Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Gerson Fraga Vieira, Wilker Henrique da Silva wote Wabrazil na Msudan, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo