Posts

Showing posts from August 18, 2018

Aliyoyasema Juma Jux baada ya kuwauzia nguo mashabiki na kupiga nao Selfie

Image
SHARE TWEET SHARE SHARE COMMENTS Siku ya August 18, 2018 msanii wa nyimbo za R&B  Juma Jux  ametumia masaa kadhaa kuwauzia mashabiki wake mavazi yenye brand yake ya  African Boy  ambapo alikuwa akipokea pesa mwenyewe na kisha kupiga nao picha mashabiki zake wote waliofika kununua bidhaa hizo za African Boy dukani kwa dada yake  Fatma  maeneo ya Sinza DSM. Bonyeza  PLAY  hapa chini kutazama  VIDEO VIDEO:  Dada wa Jux kazungumza Jux kwenda kuuza nguo dukani kwake

Kimenuka..Yabainika Kuwa Diamond Alitafuta Kiki Kupitia Safari ya South Africa

Image
Msanii wa filamu Shamsa Ford, amedai kuwa msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz alikuwa anafanya kiki kwa kudai watu watasafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kwenye sherehe ya birthday ya mtoto wake Tiffah.  VIDEO: 

Irene Uwoya 'Dogo Janja Alikurupuka tu Kutoa Wimbo wa Banana Hakuniomba Ushauri ila Sawa tu'

Image
Muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya amesema kuwa hakuombwa ushauri na mumewe ambaye ni msanii wa muziki Bongo, Dogo janja kuhusu wimbo wake wa Banana. "Ila kwa upande mmoja au mwingine naona sawa tu kwa vile ni ujumbe amefikisha ila sijui kama aliniimba mimi au Msichana mwingine, Ningeshiriki kwenye Video ile ya Banana ingebidi anilipe hela nyingi tu kwa vile na mimi nina Managment yangu na yeye ana yake" Irene

Rayvany Apingana na Boss Wake Diamond 'Sio Issue Kutoka Kimapenzi na Kila Mwanamke Staa'

Image
Mwanamuziki Rayvany ameulizwa kwanini yeye ametulia na hajawahi kusikika katika skendo mbali mbali za kutoka kimapenzi na warembo mastaa wa Bongo kama ilivyo kwa wasanii Wengine ikiwemo boss wake Diamond ambae amehusishwa katika Skendo nyingi za kutoka na Warembo Mastaa Mbali mbali, Ray Vanny Amejibu haya "Mimi naishi maisha yangu, Najichukulia kama mtu wa kawaida niko sawa na watu wote, nataka nisiishi kama mtu ambae niko dunia nyingine nikajistress, sio ujanja kuwa na Wanawake maarufu mara huyu mara huyu, sitaki kuja kujuta baadae" Rayvany

For any Customers who have a problem in laptop concerning motherboard especially in power switch and charge light if not responding

Acer Aspire V5-122P-0889 Troubleshooting The Acer Aspire V5-122P-0889 was released by Acer as a budget friendly laptop that runs Windows 8.1 . Laptop will not power on The laptop is not powering on when the power button is pressed. Power button not responding When the power button is pressed, it does not respond. If this happens, plug the laptop in to ensure that the battery is not dead. You can tell this by the light next to the charging port. If the light is on and the battery is charging, the power button may be stuck or broken. If this happens, the button may need to be removed and reseated. Battery dead If the power button is pressed and the laptop will not turn on, try plugging it in to see if it has a charge. If plugging it in doesn't work, the battery, charger, or charging port may be broken on the laptop. Dysfunctional battery Laptop batteries are made to hold a charge for a long period of time, if you start to see your battery dying quickly w...

Kwa mara ya kwanza Davido asafiri na ndege yake binafsi

Image
Msanii wa muziki kutokea nchini Nigeria, Davido mara baada ya kuweka wazi kuwa amenunua ndege binafsi, sasa ameanza kupaa nayo. August 17, 2018, Davido aliingia katika vitabu vya kumbukumbu kuanza kutumia ndege hiyo kwa mara ya kwanza. Davido ameipa ndege hiyo jina la OBO - Omo Baba Olowo (Maana yake ni Mtoto wa Tajiri) unaweza kuiita kuwa ndege ya mtoto wa tajiri, ilipaa Davido akiwa na mpenzi wake kuelekea Cotonu.

Rais wa Simba na Wenzake Kusomewa Maelezo Ya Awali Septemba 3

Image
Kesi  ya kughushi na kutakatisha Dola za Marekani 300,000 inayomkabili Rais wa  Simba, Evance Aveva, na Makamu wake, Godfrey Nyange, imepangwa kusomwa maelezo ya awali Septemba 3, mwaka huu. Jana, kesi ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi baada ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa mgonjwa. Wakili wa Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Simba lakini hakuwapo mahakamani. Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa siku saba ili upande wa Jamhuri utoe taarifa utawasomea lini washtakiwa maelezo ya awali. "Mheshimiwa Hakimu tunaomba tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali kwa sababu tayari mahakama imeamuru hati ibadilishwe washtakiwa ambao hawajakamatwa waondolewe ili kesi iendelee," alidai Nkoko. Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itasikilizwa maelezo ya awali Septemba 3. Mapema, Mahakama hiyo ilikubali upande wa Jamhuri kubadilish...

Tanzania yateuliwa rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC

Image
Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika mjini Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018, umemteua Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018 mpaka Agosti 2019. Kufuatia uteuzi huo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa 39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019.

Bill Nass Ahamia kwa Mwana FA

Image
Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'labda' amefunguka na kuweka wazi kwa jamii kuwa anatarajia kufanya mambo makubwa katika tasnia ya muziki, kwa kushirikiana na mkongwe Mwana Fa katika hilo. Billnass amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuenea picha mtandaoni ikiwaonesha marapa hao wawili wakiwa pamoja katika hali fulani ya maongezi na kupelekea mashabiki zao mbalimbali kuwa na maswali mengi juu ya hilo. "Kuna vitu vingi vikubwa kati yangu mimi na Mwana Fa, kimuziki na hata kwenye maisha mengine ya kawaida kama vile biashara na mambo mengine. Ninafanya hivyo kwasababu FA ni zaidi ya ndugu kwangu mimi ila kimuziki kuna kitu kikubwa sana kinakuja", amesema Billnass. Mbali na hilo, Billnass amesema muziki kwa sasa umekuwa biashara nzuri ndio maana huwa wanachagua watu wa kufanya nao collabo, ambao wanaamini wataweza kuwafikish...

Hizi Hapa Sababu za Trump Kujenga Kikosi Kipya cha Jeshi la Anga za Mbali

Image
Wana anga hawatapewa silaha hivi karibuni lakini kulingana na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ni kuwa China na Urusi wamekuwa wakiunda silaha za kushambulia setilaiti ambazo pia zinatakiwa kukabiliwa. Kenya yatengeneza setilaiti yake ya kwanza "Mazingira ya anga za mbali yamebadilika miaka iliyopita," alisema Pence wakati alikuwa akieleza kile kikosi hicho kipya kitafanya. Alisema kutabuniwa kikosi cha jeshi ambacho kitakuwa na majukumu ya kulinda maslahi ya Marekani kama vile setilaiti zinazotumiwa kwa mawasiano na ujasusi. The space shuttle Discovery made its final mission to the International Space Station in 2011 Rais Trump ambaye aliuzungumzia mpango huo mapema mwaka huu alionya kuhusu hatua hizo za kijeshi zimechukuliwa na washindani wa Marekani. Rais Alisema: "Nimeona vitu ambavyo hamngetaka hata kuviona." Kuna huduma za kijeshi na za kiraia kwenye anga za mbali lakini wakati mwingine zinaweza kukutana. Kijana aliyeunda setilaiti...

Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito kwa Viongozi Anaowateua

Image
Rais Magufuli amewapiga marufuku viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kuwanyang'anya bidhaa wafanyabiashara wadogo na badala yake amewaagiza viongozi wote nchini kujielekeza katika kutatua kero zinazowakabili wananchi. Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Agosti 18, 2018 alipokuwa anasalimiana na wananchi waliokusanyika mjini Sengerema akiwa njiani kuelekea Chato Mkoani Geita kwa mapumziko, ambapo mzee mmoja alidai halmashauri ya Wilaya hiyo imekuwa ikiwanyang’anya matunda aina ya nanasi wakulima na wafanyabiashara wanaouza matunda yao mjini hapo. "Nilishasema viongozi wote niliowateua mimi msisherehekee uteuzi, mtasherehekea siku mkimaliza uongozi, nataka mchape kazi, tatueni kero za wananchi na waleteeni maendeleo", amesema Dkt. Magufuli. Aidha, Dkt. Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kufuatilia na kutatua kero hiyo. Mbali na hilo, Dkt. Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa juhudi za kujenga Tanza...

Mashabiki wa Simba wapata ajali wakielekea Mwanza

Image
Gari iliyokuwa imewabeba mashabiki wa Simba tawi la Ubungo Terminal limepata ajali baada ya kumgonga mwanamke mmoja mwendesha baiskeli kisha kuacha njia maeneo ya Nzega Ndogo. Mashabiki hao walikuwa wakielekea jijini Mwanza kushuhudia mchezo wa ngao ya jamii baina ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar. Mwanamke huyo amepata majeraha na kukimbizwa hospitali wakati hakuna abiria aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo licha ya kushindwa kuendelea na safari. Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wanatarajia kushuka uwanja wa CCM Kirumba hii leo kuwakabili mabingwa wa FA klabu ya Mtibwa kwenye mchezo wa Ngao ya jamii ikiwa ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Lulu amebadilika sana, amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu – Ray C

Image
Muimbaji Ray C, amemzimikia mwigizaji wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa jinsi alivyoamua kushika dini zaidi kwa sasa. Ray C amesema Lulu amemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua, kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa. “Aisee, nimemfuatilia sana Lulu tangu ameanza kupata matatizo ya kesi yake (ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya msanii Steven Kanumba) amebadirika sana. Sasa amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu,” alisema Ray C. “Yaani nikiwa namwangalia picha zake au video zake mitandaoni anazoimba nyimbo za dini mpaka machozi yananilenga, hadi fikra zinakuja maana sikumbuki mara ya mwisho lini niliingia kanisani. “Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali. Hakika nimejifunza kitu kutoka kwake, nawashauri watu wajirudi kwa kutubu kwa mwenyezi Mungu kutokana na makosa waliyofanya, wasisubiri hadi matatizo yawapate.” Kumekuwa na video zinazosambaa mita ndaoni zikimwonyesh...

Lulu amebadilika sana, amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu – Ray C

Image
Muimbaji Ray C, amemzimikia mwigizaji wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa jinsi alivyoamua kushika dini zaidi kwa sasa. Ray C amesema Lulu amemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua, kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa. “Aisee, nimemfuatilia sana Lulu tangu ameanza kupata matatizo ya kesi yake (ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya msanii Steven Kanumba) amebadirika sana. Sasa amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu,” alisema Ray C. “Yaani nikiwa namwangalia picha zake au video zake mitandaoni anazoimba nyimbo za dini mpaka machozi yananilenga, hadi fikra zinakuja maana sikumbuki mara ya mwisho lini niliingia kanisani. “Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali. Hakika nimejifunza kitu kutoka kwake, nawashauri watu wajirudi kwa kutubu kwa mwenyezi Mungu kutokana na makosa waliyofanya, wasisubiri hadi matatizo yawapate.” Kumekuwa na video zinazosambaa mita ndaoni zikimwonyesh...

Usain Bolt kuitumikia klabu ya Central Coast Mariners

Image
Mwanariadha anaeaminika kuwa na kasi zaidi duniani, Usain Bolt ametua jijini Sydney  nchini Australia asubuhi ya leo tayari kwaajili ya majaribio kabla ya kujiunga na klabu ya Central Coast Mariners. Bolt amedhamiria kweli kutimiza ndoto zake katika mchezo wa soka baada ya kutua Sydney kukamilisha dili hilo ndani ya timu ya Central Coast Mariners inayoshiriki A-League ya nchini Australia. Bingwa huyo mara nane wa michuano ya Olympic ameeleza hamu yake kuhamia upande wa soka mara baada ya kustaafu mchezo wa riadha na kusisitiza kuwa atabaki Australia kwa muda wake wote. Raia huyo wa Jamaica mwenye umri wa miaka  31, tayari ameshafanya mazoezi ya soka na klabu kama Borussia Dortmund, Stromgodset na Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini.

TANZIA: Kofi Annan afariki dunia

Image
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amefariki dunia leo Agosti 18, 2018 nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mwanadiplomasia huyo kutoka Ghana, Annan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 huku akiwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1997 na 2006. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi baada ya kifo cha Annan huku akimwagia sifa kuwa alikuwa msimamizi elekezi wa mema.

Simba yaipiga Mtibwa Sugar na kutwaa Ngao ya Jamii

Image
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa Ngao ya jamii uliyopigwa CCM Kirumba Mwanza. Simba imepata mabao yake kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga dakika ya 29 na Hassan Dilunga 45+3 wakati bao pekee la Mtibwa Sugar likifungwa na Kelvin Kongwe 33. Kukamilika kwa mchezo huo ni ishara sasa ya kufunguliwa rasmi kwa michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara inayorajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22.

Exclusive: EFM waeleza kwanini wamempiga ‘stop’ Mavoko kwenye Komaa Concert 2018 licha ya kumtangaza (Video)

Muimbaji, Rich Mavoko ameshindwa kufanya show yake ya kwanza ndani ya tamasha la Komaa Concert 2018 jijini Dar es salaam toka aondoke WCB baada ya uongozi wa EFM kuamua kusitisha asifanye show licha ya kumtangaza kwamba atakuwa kwenye tamasha hilo liliohudhuriwa na watu 30000.

Naomba Mungu ipo siku nitaacha muziki, nataka tu kuacha nimpumzike kabisa – Mr Blue

Muda wowote kuanzia sasa hivi huwenda rapa mwenye mafanikio makubwa katika muziki wa Hip Hop, Mr Blue akaacha kufanya kabisa muziki. Amesema mke wake amekuwa akimshauri hivyo kwa muda mrefu kitu ambacho kimemfanya aanze kufikiria kuchukua uamuzi wa kuachana na muziki ili aswali.

RayVanny: Sio ishu kutoka kimapenzi na kila staa, sitaki nije nijute baadae (Video)

Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny amesema hataki kabisa ishu za kubadili wasichana kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wa muziki. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anakaa na mpenzi wake pamoja na mtoto wake mmoja, ameiambia Bongo5 kwamba ataishi maisha yake ili asije kujuta huku baadaye.

Nikiamua kufanya umalaya nafanya kweli – Amber Lulu

Msanii wa muziki, Amber Lulu amefunguka kwa kudai kwamba kuna wakati anaamua kufanya umalaya lakini kwa sasa ameachana na mambo hayo. Muimbaji huyo ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliopamba tamasha la Komaa Concert la EFM, amedai kwa sasa ameamua kufanya muziki na kuacha mambo mengine.