NancyTheDreamtz Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema atalifikisha Mahakama Kuu suala la gharama za matibabu yake ili iweze kutoa tafsiri sahihi baada ya Bunge kushindwa kumlipia. Lissu aliyasema hayo kupitia andiko lake lililoanza kusambaa jana akiwa anatimiza mwaka mmoja tangu alipopigwa risasi Septemba 7, mwaka jana eneo la nyumbani kwake jijini Dodoma. Katika andiko lake hilo ambalo pia ameelezea tukio zima la kujeruhiwa kwake, mwenendo wa matibabu katika kipindi chote cha mwaka mmoja na kile alichodai kiini cha kuumizwa kwake, kuhusu suala la matibabu ambalo amelifafanua kwa kina Lissu ametoa sababu za kimazingira na kisheria ambazo ndio msingi wa yeye kuamua kulifikisha suala hilo mahakamani. “Kwa upande wetu, njia pekee iliyobaki sasa ni kulipeleka suala hili mahakamani ili Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya jambo hili. Maandalizi ya kwenda mahakamani yanaendelea,” alisema Lissu. Akirejea mvutano kuhusu Bun...