Ommy Dimpoz Kafunguka Kila Kitu Kuhusu Ugonjwa Wake....Anasema Alilishwa Sumu Bila Kujua
NancyTheDreamtz Vipimo vya afya alivyofanyiwa msanii wa Bongofleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu, vimeonyesha aliwekewa sumu kwenye chakula. Ommy Dimpoz alianza kuugua mapema Mei mwaka huu na kwenda kutibiwa mjini Mombasa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini ambako aligundulika kuwa na tatizo katika njia ya chakula ambako alifanyiwa upasuaji. Akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds, Dimpoz, alisema vipimo vya madaktari vimeonyesha tatizo lake linatokana na kuwekewa sumu kwenye chakula ama kinywaji. “Awali nilifanyiwa vipimo katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam na kugundulika nina kansa, lakini baada ya vipimo vikubwa huku Afrika Kusini, imeonekana nimekula sumu,” alisema Ommy Dimpoz. Alisema anashukuru kuona hali yake imeanza kuimarika baada ya awali kushindwa kuzungumza kabisa na anaamini sala za Watanzania wenzake na watu ambao wamekuwa karibu naye zitamsaidia na kuweza kurejea kwenye hali y...