Posts

Showing posts from October 23, 2019

‘Ugonjwa wa Zari’ Wahamia Kwa Mama Diamond

Image
NancyTheDreamtz ULE ‘ugonjwa’ wa show-off (kujionesha na kuringishia) magari ya kifahari anaodaiwa kuwa nao mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, umehamia kwa mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama D’. Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi amekuwa akisifika kwa kutupia picha mitandaoni akipozi na magari makali ikielezwa kuwa huwa analenga kuwarusha roho mahasimu wake. Sasa ishu hiyo imehamia kwa Mama D au Mama Dangote ambaye naye kwa siku kadhaa amekuwa akitupia picha za magari ya kifahari yanayomilikiwa na familia yake. Mama Dangote naye inasemekana amekuwa akifanya hivyo kama sehemu ya kuwaziba midomo wanaozusha mambo mengi kuhusu familia yake. Kwa sasa Mama Dangote siyo yule wa zamani aliyeonekana kutoka familia isiyokuwa vizuri kipesa ambapo sasa ‘anakomoa’ baada ya mwanaye kupata utajiri. Mama Dangote na Mondi wamekuwa bega kwa bega tangu staa huyo alipoanza kupata umaarufu yapata

Mbwana Samatta arahisishiwa kazi kwa mabeki wa Liverpool

Image
NancyTheDreamtz Mshambuliajiwa KRC Genk, Mbwana Samatta atakuwa katika wakati mzuri wa kuonesha uwezo wake mbele ya mabingwa watetezi wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, Liverpool baada ya safu yao ya ulinzi kupungua nguvu. Mchezo huo wa tatu hatua ya makundi unatarajia kupigwa leo katika uwanja wa Luminius Arena mjini Genk, nchini Ubelgiji, ambako ndiyo maskani ya klabu hiyo anayokipiga nahodha wa Taifa Stars. Taarifa zilizopo hii leo zinaeleza kuwa mlinzi machachari wa upande wa kulia wa Liverpool, Trent-Alexander Anold hajafanya mazoezi na klabu yake kutokana na kukumbwa na homa, hivyo hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Genk. Genk ya Mbwana Samatta iko katika kundi E ikiwa na pointi moja katika nafasi ya mwisho baada ya kufungwa mechi moja na kutoka sare mechi moja. Napoli inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, huku Liverpool ikiwa na pointi 3 katika nafasi ya pili na Red Bull Salzburg ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 3.

WhatsApp Yamponza Askari Magereza Apolwa Siraha Kisa Kuchart

Image
NancyTheDreamtz Askari wa Jeshi la Magereza nchini Uganda wanachunguza tukio la Afisa Mwanamke wa Gereza aliyeibiwa silaha ya kivita aina ya AK-47 wakati akiwa katika Gereza la Mpigi. Afisa aliyeibiwa ametambulika kwa majina ya Hadijah Katono ambaye imeelezwa kuwa wakati akiibiwa silaha hiyo alikuwa akipiga soga katika mtandao wa WhatsApp. Mashuhuda wameeleza kuwa kijana mmoja aliyekuwa ameshika mkuki alimshambulia afisa huyo kwa kumpiga mara mara kisha akachukua silaha na kutimua mbio.

Simba na Azam Kibaruani Leo Kusaka Point Tatu

Image
NancyTheDreamtz LEO uwanja wa Taifa Simba na Azam zitakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu. Wachezaji wanne wataukosa mchezo huu kutokana na sababu mbalimbali ambapo kwa Simba nyota hawa watakosekana leo John Bocco ameanza mazoezi mepesi ila leo hatacheza kwa kuwa hayupo fiti. Jonas Mkude na Mohamed Hussein 'Tshabalala' wanatibu majeraha waliyoyapata kwenye timu ya Taifa. Kocha Mkuu wa Simba, Patric Aussems amesema kuwa atatafuta mbadala wao kwani ana kikosi kipana. Kwa upande wa Azam FC wao hawana majeruhi kabisa isipokuwa ni maamuzi ya Kocha kuamua kumtumia nahodha Agrey Moris ambaye ametoka kupona majeraha yake muda si mrefu. NOMA ZAIDI YA NOMA TAZAMA ROSA REE ALICHOKIFANYA KWA VIDEO:

IRENE Uwoya "Roho Inaniume Sana Kwa Mwanangu Kutukanwa Mitandaoni"

Image
NancyTheDreamtz "Hakuna kitu kinachoniuma kama kutukaniwa mwanangu huwa naumia sana inafikia kipindi naogopa kumpost mitandoni japo Krish mwenyewe huwa nachukia nisipopost picha yake" Ameyasema hayo UWOYA alipoojiwa na Zamaradi

Top 5 ya Wasanii Matajiri Africa, Diamond Hayupo...Why?

Image
NancyTheDreamtz Mimi sio shabiki wa mambo ya muziki wa Tanzania, ila napenda sana kuingia mitandaoni na sifa anazopewa Diamond ni nyingi sana. Ila nimejiuliza, baada ya pitapita zangu nimekutana jarida maarufu Marekani la Forbes limetaja wasanii matajiri zaidi Barani Africa ila cha kushangaza Diamond sijamuona kabisa, shida nini? Nikaendelea kucheki hadi Top-Ten jamaa hayupo ila Wizkid & Davido wapo. Au uwa ni kiki tu na maisha ya kuigiza