Posts

Showing posts from August 4, 2020

Utata Waibuka Msanii Mpya wa Harmonize!

Image
UTATA umeibuka baada ya bosi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, mwanamuziki Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’ kumtangaza msanii mpya wa lebo hiyo, Raoul John Njeng-Njeng ‘Skales’ kutoka nchini Mwishoni mwa wiki iliyopita, Harmo alitangaza kumsaini msanii wake mpya, Skales baada ya Ibrahim Abdallah ‘Ibraah’ aliyemsaini mapema mwaka huu, hivyo kufi kisha idadi ya wasanii wake wawili.   Harmo aliweka posti kwenye ukurasa wake wa Instagram akimkaribisha Skales kwenye Lebo ya Konde Gang; “We are happy to welcome genius musician from Nigeria, my brother @youngskales welcome to the family @ kondegang is a dream team.”   Baada ya kutangaza kumsaini Skales kama msanii wake, ndipo utata ukaibuka kufuatia staa huyo wa Nigeria kusema kuwa hajasainiwa kama msanii wa Konde Gang, bali lebo hiyo itahusika kusimamia kazi zake kwa ukanda wa Afrika Mashariki.   “Hello my East African lovers, i have offi cially come on board with Konde Music, the team will now stand as my management in East Africa,’’

Jide: Zuchu Atafika Mbali!

Image
MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ amesema kuwa msanii na memba mpya wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’, atafika mbali kutokana na juhudi zake.   Akizungumza na OVER THE WEEKEND, Jide amesema, Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.   “Zuchu ana juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake, kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi (Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’ amesema Jide. NancyTheDreamtz

Warembo Waliotikisa Ubunge Viti Maalum

Image
  KINYANG’ANYIRO cha kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana CCM (UV-CCM), kimeendelea kutikisa baada ya mchakato huo ulioanza mwishoni mwa wiki, kushuhudia sura mpya za walimbwende zilizoibua gumzo nchini.   Katika mchuano huo, wajumbe wa UVCCM katika kila mkoa, walipiga kura za maoni kuchagua wawakilishi wao, ambao watapata fursa ya kupeperusha bendera ya CCM baada ya uchaguzi mkuu kufi kia tamati Oktoba 28 mwaka huu.   Katika uchaguzi huo, mbali na wanawake hao kuwa na umri mdogo, lakini kivutio kingine kilichoibua mtikisiko wa kipekee katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ni urembo walionao washindi hao.   Baadhi ya wachangiaji katika mitandao hiyo, walihoji iwapo mojawapo ya vigezo katika nafasi hiyo ni kuwa mlimwende, jambo ambalo lilikanushwa na baadhi ya viongozi waliozungumza na IJUMAA Wikienda.   “Si kweli kuwa urembo ndiyo kigezo, cha msingi tunazingatia elimu kwa mujibu wa taratibu, uweledi na uzalendo kwa maana ya kuwa na uwezo wa kujieleza, kutete

Meninah Apewa Makavu Laivu!

Image
MSANII wa muziki, filamu na mshehereshaji maarufu  Bongo ,  Meninah Attick , amepewa makavu laivu baada ya kuposti  video  kwenye ukurasa wake wa  Instagram  akiwa anafanyiwa masaji na mwanaume.   Meninah aliposti video hiyo akifanyiwa masaji na mwanaume asiyejulikana, jambo ambalo liliwakera wafuasi wake waliosema kwamba, anarudia yaleyale ya mwaka jana.   Baadhi ya wafuasi hao walimshambulia kwa kusema kuwa mambo mengine anajitakia mwenyewe. “Huyu mwanamke sijui huwa hajielewi? Anajirekodi mwenyewe video zake halafu anakuwa wa kwanza kukimbilia Polisi na kuwaletea shida watu wengine,” aliandika mmoja wa wafuasi wake anajiita Saraatz.   Oktoba 10 , mwaka jana,  Meninah  aliitwa na  Baraza la Sanaa Taifa  ( Basata ) kwa kuhusishwa na kosa la kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo lilimuingiza matatani mwigizaji na komediani  Burton Mwemba ‘Mwijaku ’ ambaye mpaka sasa ana kesi ya  Makosa ya Mtandao. NancyTheDreamtz

Dah! Stori ya Kanye West Inauma Sana Aisee!

Image
HAINA ubishi, Rapa bilionea, Kanye West ni miongoni mwa marapa bora kuwahi kutokea duniani.  Jamaa ni bonge moja la mwimbaji kutoka pale Atlanta nchini Marekani.   Ni prodyuza wa muziki wa Hip Hop. Anashikilia rekodi kibao kwenye mauzo ya muziki wake ambao umeuza nakala nyingi zaidi na kumfanya kupendwa sehemu kubwa ya Sayari ya Dunia, huku akiingiza mkwanja wa kutisha.   Anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani bilioni 1.3 (zaidi ya shilingi trilioni 2 za Kitanzania) akiwa nyuma ya Jay-Z. Ripoti za thamani za wanamuziki duniani zinaonesha kuwa, ukimtaka Kanye West kwa ajili ya shoo kwa baadhi ya mabara kama Ulaya na Afrika (ikiwemo Tanzania), siyo chini ya Dola za Kimarekani laki 5 (zaidi ya shilingi bilioni moja za madafu).   Kanye West amesikika kwa miongo mitatu sasa kwenye ngoma nyingi. Baadhi ya ngoma za Kanye West zilizoweka rekodi nyingi duniani ni pamoja na Otis, Power, Forever, Fade, Good Life, Jesus is King, Jesus is Born na nyingine kibao.   Ndoa yake na supastaa wa T

Mbowe ashtukia muungano kama UKAWA, ni baada ya kumpitisha Lissu urais 2020

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu, kitafanya maamuzi kwa tahadhari kuhusu kuungana na vyama vingine vya upinzani. Mbowe ameeleza kuwa wamesikia wito wa vyama vingine vikiwataka kuungana, lakini hawatafanya hivyo kama mtindo tu bali wataangalia maslahi mapana ya chama chao. Ajira: Nafasi za kazi kwa watangazaji, waandishi wa habari Aliyasema hayo jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, baada ya chama hicho kumpitisha Naibu Mwenyekiti wake, Tundu Lissu kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 28, 2020. Lissu aliwashinda waombaji wengine wa nafasi hiyo ambao ni Lazaro Nyalandu na Maryrose Majige. Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa Chadema imekuja siku kadhaa baada ya Chama Cha ACT-Wazalendo ambacho kimempitisha Bernard Membe kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais wa Zanzibar, kuomba washirikiane ili waweke mgombea m

Wasanii wa Filamu nchini watakiwa kufanya kazi zenye ubora

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wasani wa filamu nchini kufanya kazi zenye ubora na viwango vya juu ili kuboresha maslahi yao maslahi yao na kushindana na soko la nje. Akizungumza na wadau wa filamu nchini wakati wa uzinduzi wa kanuni mpya za Bodi ya filamu nchini, Waziri Mwakyembe amewataka wasanii kutumia maboresho ya kanuni hizo kwa kufanya kazi zenye ubora na viwango vya juu katika soko la ushindani. “Ni wakati sasa kwa wasanii wa filamu nchini kufanya kazi nzuri kwani kanuni hizi zimepunguza tozo na ada mbalimbali kwa kiwango kikubwa lengo likiwa ni kumuwezesha msanii wa filamu nchini kufanya kazi katika mazingira mazuri,” alisema Waziri Dkt. Mwakyembe. Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini, Profesa Frown Nyoni amesema kuwa kuanza kutumika kwa kanuni hizi kutapanua wigo kwa wasanii nchini kuongeza kipato kwani kila kazi ya msanii itakuwa ikilipiwa katika vyombo vya habari. Kwa upande wake msanii mkongwe nchini Ahm

Mkwassa Apigwa Chini Yanga

Image
Kamati ya ufundi ya klabu ya Yanga imefanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi la kalbu hiyo kwa kuacha na kocha msaidizi Boniface Mkwassa na kuwapangia majukumu mengine baadhi ya watendaji wa benchi hilo. Uamuzi wa Yanga umetangazwa leo na mwenyekiti wa kamati hiyo Dominick Albunis kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kiundetaji wa klabu hiyo. Kwenye taarifa iliyotolewa na Yanga wengine walitolewa kwenye benchi la ufundi ni kocha wa makipa Peter Manyika na meneja wa timu Abeid Mziba, kit manager Fred Mbuna ambao kwa pamoja watapangiwa Majukumu mengine. NancyTheDreamtz