Posts

Showing posts from November 1, 2018

Yanga kuweka hadharani mchakato wa Uchaguzi Leo

Image
NancyTheDreamtz Wakati klabu ya Simba ikielekea kufanya Uchaguzi wake mkuu Novemba 4 2018, Uongozi wa Yanga nao umetangaza kuweka hadharani mchakato wa Uchaguzi wao leo. Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu, Omar Kaya, ameeleza kuwa uongozi utaeleza kila kitu kuhusiana na uchaguzi utakaofanyika kama utakuwa ni Mkuu ama wa kujaza nafasi. Kaya ameeleza hivyo kutokana na matamko tofauti tofauti ya klabu hiyo siku zilizopita kusema watafanya uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo zipo wazi baada ya viongozi kadhaa kujiuzulu. Viongozi kadhaa akiwemo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, pia aliyekuwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa, waliachia ngazi na nafasi zao zikiendelea kuwa wazi mpaka sasa. Mbali na nyadhifa hizo zilizo wazi, Yanga pia ilitoa matamko ya kueleza nafasi ya Mwenyekiti wao Yusuf Manji, itaendelea kuwepo kufuatia mkutano mkuu wa mwisho uliofanyika Juni 6 2018 kuamua Manji aendelee kukalia kiti hicho.

FIFA Yamfungia Maisha Rais wa Chama cha Soka Ghana

Image
NancyTheDreamtz Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo Alhamisi ya November 1 2018 zimeripotiwa taarifa za kumfungia rasmi maisha kujihusisha na soka aliyekuwa Rais wa chama cha soka Ghana Kwesi Nyantakyi. FIFA imetangaza kufikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa Kwesi alitenda kosa la kupokea rushwa kinyume na taratibu za kazi yake kutoka kwa muandishi wa habari za uchunguzi. Kwesi amekutwa na hatia ya kuokea rushwa ya zaidi ya Tsh Milioni 149 kutoka kwa mwanahabaribari aliyekuwa anafanya habari za uchunguzi wa ufisadi na rushwa katika mchezo wa soka.

Polisi Wapekua Nyumbani kwa Zitto Kabwe

Image
NancyTheDreamtz Polisi wamefanya upekuzi nyumbani kwa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe  na kumrudisha katika kituo cha Oysterbay kutoka Kituo Kikuu Wakili wa Mbunge Huyo Jebra Kambole amesema polisi wamefika nyumbani kwa mteja wake Maeneo ya Masaki Jijini Dar es Salaam na Kufanya upekuzi. Kambole ameeleza kuwa baada ya kukamatwa alipelekwa oysterbey polisi ambapo baadaye alihamishiwa kituo kikubwa cha polisi na hakulala hapo alihamishiwa kituo cha mburahati.

Kagere Afunguka Kuhusu Mabao Anayofunga Okwi

Image
NancyTheDreamtz Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda, amemfungukia mshambuliaji mwenzake Emmanuel Okwi na kusema kuwa anafurahi kuona anafunga. Okwi kwa sasa ana mabao 7 kwenye ligi akiwa nafasi ya pili mbele ya Eliud Ambokile mwenye mabao 8 huku Kagere akiwa na mabao matano. "Nimefurahi kuona Okwi anaendelea kufunga kwani sisi wote ni washambuliaji wa Simba, tuna jukumu moja la kuisaidia timu ifanye vyema hivyo  yeye akifunga na mimi nitafunga ni jambo jema ambapo inatusaidia sisi kutwaa ubingwa msimu huu, mimi sina shida," alisema. Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 23 Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Lipuli FC, wamefikisha pointi 25 huku vinara wakiwa ni Azam FC wenye pointi 27.

Breaking News: Wema Sepetu Asomewa Mashtaka ya Kusambaza Video ya Ngono Aachiwa kwa Dhamana

Image
NancyTheDreamtz MSANII wa Filamu nchini, Wema Sepetu leo Novemba 1, 2018 amepandishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisitu akikabiliwa na shtaka la kusambaza video yake isiyo na maadili (video za ngono) kupitia mitandao ya kijamii (Instagram). Wema amesomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Saanane Kasonde ambapo amekana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Tsh. Milioni 10 baada ya kupata mdhamini, Salim Limu ammbaye amekamilisha taratibu za dhamana hiyo. Aidha, Wema ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wake, Reuben Simwanza ametakiwa asiposti video/picha yoyote isiyo na maadili au inayoashiria ngono kwenye mitandao yake na kesi hiyo ikiahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu. Akizunngumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TCRA, Joannes Karungura amesema; “TCRA tupo makini, tunapenda kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na picha na video za hamna hiyo wazifute katika simu zao, kwa sababu hairuhusiwi wala kuposti kokote kuanzia sasa na kuendel

Chris Brown Aweka Mambo Sawa na Mzazi Mwenzie Kuhusu Matunzo ya Mtoto

Image
NancyTheDreamtz Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Chris Brown pamoja na mzazi mwenza Nia Guzman kuwa wako sawa kwa sasa kwenye suala zima la utoaji matunzo kwa mtoto wao Royalty baada ya kupelekana mahakamani miezi kadhaa iliyopita. Inaelezwa kuwa Chris Brown yupo mbioni kumnunulia Nia Guzman nyumba mpya atakayokuwa akiishi na mtoto wao Royalty mwenye umri wa miaka minne pamoja na kulipa kiasi cha zaidi ya Tsh Bilioni 2 kwaajili ya mwanasheria wa Nia Guzman. Miezi kadhaa iliyopita Nia Guzman aliiambia Mahakama kuwa alitaka kiasi cha zaidi ya Tshs Millioni 48 kila mwezi kwaajili ya matumizi ingawa Chris Brown alikua akitoa Tsh Millioni 5 kila mwezi, Inadaiwa kuwa wawili hao wapo katika harakati za kufuta mashtaka yanayowakabili Mahakamani baada ya miezi kadhaa kupita kuonekana kwa Chris Brown na Nia Guzman kuwa katika hali ya kuelewana kwaajili ya mtoto wao.

Magufuli Ataja Fedha za Ndege Zilipotoka

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema serikali imeweza kununua ndege kwa mara moja ni kutokana na fedha ambazo zimetokana na serikali kuwabana mafisadi. Akizungumza wakati wa uchangiaji kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake ambapo alitaja chanzo cha fedha hizo. “Mengine tumenunua ndege, kwa sababu watalii wetu walikuwa wachache, huwezi ukategemea shirika la ndege la jirani kuleta watalii kwenye nchi yako, tumeamua na ndio maana tumenunua ndege saba, hatukukopa nchi yoyote”, amesema Rais Magufuli “Ni hizi hizi fedha tulizowabana mafisadi ndio tumenunua ndege, unambana fisadi anaendelea kulia kule lakini fedha unepeleka kwenye ndege wananchi wengine wananufaika, na ukilipa kwa mkupuo gharama inakuwa ndogo”, ameongeza. Aidha Rais Magufuli kwa kipindi cha miaka mitatu serikali imefanikiwa kushughulikia masuala mbalimbali, ikiwemo utoaji wa elimu bure, na kuimarisha hali ya u

Yanga Yafunguka Kuhusu Mchezaji wao Ibrahim Ajibu

Image
NancyTheDreamtz Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuwa huenda nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu amegoma kucheza kwasababu ya kutolipwa mshahara, hatimae klabu ya Yanga imethibitisha kuwa nyota wake amerejea mazoezini baada ya kupona kutokana na majeraha. Yanga ambayo ilitoa mapumziko kwa wachezaji wake baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Lipuli FC imethibitisha kuwa leo wamchezaji wamerejea mazoezini na moja ya wachezaji walioanza mazoezi leo ni Ibrahim Ajibu na. ''Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi kimerejea mazoezini tayari kwa mchezo wa jumapili dhidi ya Ndanda Fc. Mchezaji Ibrahim Ajibu amerejea kikosini na amefanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wa Ndanda FC'', imeeleza taarifa ya Yanga. Ajibu hajaonekana uwanjani kwenye michezo miwili ya Yanga kati ya KMC na Lipuli FC ambapo mchezo wake wa mwisho kucheza ilikuwa ni dhidi ya Alliance FC, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Baada ya mchezo huo Yanga ilitoa taarifa kuwa Ajibu alikuwa akisumbuliw

Mbowe Apelekwa Nje ya Nchi kwa Matibabu

Image
NancyTheDreamtz Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Akiieleza mahakama mdhamini wa mbowe amedaiwa kuwa ameelezwa na mke wa Mbowe kuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na shinikizo la damu. Kufuatia maelezo hayo wakili wa serikali ameiomba mahakama kutoa amri ya kumkamata mbowe ili ajieleze kwa nini dhamana aliyopewa na mahakama kwanini isifutwe kwa kushindwa kufika mahakamani

Rais Magufuli: Nilifunga Ndoa Bila Koti la Suti, Mke Wangu Bila Gauni la Bi Harusi nilikunywa Pepsi ye Alikunywa Milinda

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Tanzania John Magufuli leo amesema alifunga ndoa bila kuvaa koti la suti na mkewe Janeth hakuvaa gauni la bibi harusi. Ndoa hiyo ilifungwa wakati Magufuli akiwa mwanafunzi katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na haikuambatana na sherehe yoyote. Akiongea leo katika mdahalo uliofanyika UDSM kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake wan chi, Magufuli amesema amefurahi kurudi chuoni hapo ambapo si tu alipata elimu yake ya juu bali kufunga pingu za maisha. "Siku niliyooa watu wengi hawakujua…na haimaanishi sikuwa na pesa ya kununua koti au gauni la harusi kwa mke wangu, sikuona kama vitu hivyo ni vya msingi sana." "Tulienda hapo kanisani pete tukanunuliwa na Padre, tena zilikuwa za shaba. Padre pia alitununulia soda, nakumbuka mimi nilikunya pepsi na mke wangu alikunya mirinda...Baada ya hapo nikaendelea na shughuli zangu." Padre ambaye aliwafungisha ndoa hiyo na kutoa ufadhili wa pete na soda kwamujibu wa Rais Magufuli anaitwa M

VIDEO:Tazama RC Makonda Alivyowatangaza Baadhi ya Mashoga...James Delicious Atajwa na Wengi

Image
NancyTheDreamtz Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameunda Kamati ya watu 17 ya kuchunguza masuala mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya vijana wa Mkoa huo kinyume na sheria na desturi za nchi ikiwemo ushoga na kurekodi video za ngono kisha kuzisambaza. Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku tangu alipowataka wakazi wa Dar kumtumia majina ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo baada ya video ya msanii Amber Rutty kusambaa mitandaoni akifanya mapenzi kinyume cha maumbile. “Kitendo cha kumuingilia mtu kinyume cha maumbile ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya taifa letu, lakini kuna watu wanajiuza kwenye mitandao na wanaona kwao ni jambo la kawaida, hii ni aibu kubwa. “Mpaka sasa nimepokea meseji 18972, sio mchezo, wote wanalaani, majina 200 ni ya mashoga, mengine yanajirudia kama James Delicious, Dida Mtamu, Anti-Miliki na makundi ya ngono ya WhatsApp kama #PachuPachu wote wametajwa. Endeleen

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Ligi Kuu Ubelgiji...Atupia Tena Mawili

Image
NancyTheDreamtz Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta anazidi kuwa tishio kwa magolikipa katika michuano ya Ligi Kuu Ubelgiji na Europa League, usiku wa October 31 KRC Genk walikuwa ugenini kucheza game yao ya 13 ya Ligi Kuu Ubelgiji (Jupiter Pro League) dhidi ya Antwerp FC. KRC Genk wakiwa ugenini licha ya kutanguliwa kwa magoli 2-0, walifanikiwa kusawazisha magoli yote na Mbwana Samatta akafunga magoli mawili ya ushindi dakika ya 76 na 90 baada ya Ruslan Malinovsky kuisawazishia Genk magoli ya mawili ya mwanzo kwa mikwaju miwili ya penati aliyofunga dakika ya 56 na 60, magoli pekee ya Antwerp yakifungwa na Bolingi dakika ya 23 na Jukleroed dakika ya 45. Ushindi huo umeifanya Genk kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha jumla ya point 33 wakifuatiwa na Club Brugge waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 30, wakati Antwerp wapo nafasi ya tatu kwa kubaki na point zao 25, S

Tanzania Tujifunze kujiajiri na sio kuajiriwa 2018

Image
NancyTheDreamtz Kijana Arthur Raphael Nyandiche ni kijana ambaye ameamua kujiajiri mwenyewe kupitia Taaluma yake ya Commerce na Computer aliyopitia miaka kumi iliyopita nyuma na kuweza kujipatia kipato chake mwenyewe, kijana anafanya kazi kwa bidii na utiifu kwalengo la kutimiza ndoto zake hasa katika masuala ya Computer Software,Hardware,Networking,Graphics and Design pamoja na masuala ya kutengeneza wavuti na tovuti za makampuni mbalimbali kupitia hilo yeye ameweza kutambulika na watu mbalimbali nje na ndani ya Nchi ya Tanzania.Hivyo basi kijana anawaasa vijana wanaohitimu elimu ya vyuo sasa kujikita katika ajira binafsi badala ya kuitegemea Serikali ndio iweze kutoa Ajira kwa watanzania wote watakao hitimu lazima wengine watengeneze ajira za watu wengine Kijana anajichanganya pia katika masuala ya Kijamii kupitia serikali kama unavyoona picha tofauti ambazo kijana Arthur anazifanya kama picha baadhi hapo zinaonesha kumbukizi za mwalimu nyerere wilayani nanyumbu a