Ifahamu Kemikali Iliyoisambaratisha Beirut
TAKRIBANI tani 3,000 za kemikali ya ammonium nitrate zilizohifadhiwa miaka sita iliyopita katika ghala zimeelezewa kusababisha mlipuko huo uliotokea katika jiji la Beirut ambayo ni bandari na mji kuu wa Lebanon siku ya Jumanne. Lakini ammonium nitrate ni nini na kwa nini inaweza kuwa kemikali hatari? Ammonium nitrate (NH4NO3) ni kemikali iliyo na umbo la madonge meupe ambayo hutengenezwa viwandani. Matumizi yake huwa ni chanzo cha naitrojeni kwa ajili ya mbolea, lakini pia inatumika kwa ajili ya kutengeneza vilipuzi kwa ajili ya migodi. Kemikali hii hutengenezwa duniani kote na ni rahisi kuinunua. Lakini utunzaji wake unaweza kuwa tatizo, na kemikali hii imekuwa chanzo cha ajali kadhaa za viwandani miaka ya nyuma. Ammonium nitrate ni hatari kwa kiasi gani? Yenyewe ilivyo, ni salama, anasema profesa wa kemia, Andrea Sella, kutoka shule ya sayansi ya Chuo Kikuu cha London. Hata hivyo, ukiwa na kiasi kikubwa cha kemikali hiyo kwa muda mrefu, huanza kuoza. ”Tatizo ni kwamba kadiri muda u