Posts

Showing posts from October 4, 2018

Picha ya Wanjara na Mwanamke Mwenzie Yazua Utata

Image
NancyTheDreamtz Mwanadada Rashida Wanjara ambae aliwahi kushiriki taji la miss tanzania mwaka 2000 alikumbwa na tetesi za kuwa na tabia zisizo sawa baada ya kuonekana katika picha zilizosambaa mitandaoni akiwa na mwanamke mwenzake wakiwa katika pozi tata. Hata hivyo mwanadada huyo anaonekana kutokujali kuhusu maneno hayo na kusema kuwa hawezi kuwazuia watu kufikiria vile wanavyotaka kufikiria hata siku moja. Huwezi kuwazuia watu kufikiria vile wanavyofikiria kwa sababu kumbusu mwanamke mwenzangu wala sio kosa, na ni kitu cha kawaida sana na hakuja jambo baya wala la ajabu na hakuna cha zaidi Hii imekuwa ni tabia ya mastaa wengi wa kike kupiga picha tata na wanawake wenzao kitendo kinachowafanya mashabiki kupoteza imani nao.

Baada ya Mambo Kumwendea Hovyo Dogo Janja kaamua Kukimbilia kwa Mwanasaikolojia

Image
NancyTheDreamtz Inasemekana Dogo Janja hayuko sawa Kisaikolojia hii ni baada ya kupost picha kupitia ukurasa wake wa instagram akiwa na mwanasaikolojia maarufu nchini Chris Mauki. Wengi wamedai  sababu ya Dogo Janja kukutana na mwanasaikolojia huyo ni kuwekwa sawa  yale yote anayopitia kwa sasa kutokana na wengi kuhusisha kuwa kuna ugomvi  unaendelea kati yake na mke wake Irene Uwoya kitu hicho kinamfanya asiwe katika hali yake ya kawaida. Dogo Janja ameandika  “Shukrani sana kaka @chrismaukiphd 🙏🏻 ni furaha kuwa na watu kama nyingi”

Aunt Ezekiel Azungumzia Penzi Lake na Mose Iyobo

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa Filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuhusu maisha yake ya kimahusiano na Mose Iyobo ambaye pia ni dancer wa msanii Diamond Platnumz. Aunt amesema kuwa wanapokuwa kwenye familia anasahau kabisa iwapo mumewe ni dancer kwani anapokuwa ndani anabeba majukumu kama baba. "Huwezi kuamini kuna time nasahau kama ni dancer kwa sababu anaporudi nyumbani u-dancer anaacha njee, akifika ndani anakuwa baba, na hivi anavyosafiri ndio sijui kabisa kama anacheza au nini," Aunt ameiambia Wasafi TV. Aunt Ezekiel na Mose Iyobo wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Cookie ambaye ni miongoni mwa watoto wanaofuatiliwa zaidi kwenye mtandao wa Instagram akiwa na followers zaidi ya laki nne.

Kwa Hili Alilofanya Diamond Namibia Natabiri Mafuriko Wasafi Festival Bongo...

Image
NancyTheDreamtz Ukitazama hii Video hapa chini ndo utajua ukubwa wa Diamond Platnumz, Hapo ni nchini Namibia week iliyopita ambapo aliweza kujaza nyomi la hatari , shangwe hilo sijawahi liona hata kwenye show zetu za Kubwa za Fiesta Hapa Tanzania, Diamond Mwenyewe ametangaza ujio wa Tamasha la Wasafi Festival Hapa Tanzania na Kenya.... Tazama VIDEO:

MAHABA NIUWE: Kanye West amlipa Kim Kardashian Tsh bilioni 2 kulinda penzi lake

Image
NancyTheDreamtz Rapper Kanye West imemlazimu kumlipa mke wake Kim Kardashian kiasi cha dola milioni $1 ambayo ni sawa na Tsh bilioni 2 baada ya kumzuia mke wake kuposti picha moja ya tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram. Kanye West na Kim West Kim akiwa kwenye mahojiano ya uzinduzi wa Podcast ya mtangazaji maarufu nchini Marekani,  Ashley Graham ‘Pretty Big Deal’, Kim amesema kuwa wiki moja kabla ya siku ya Mama duniani alitafutwa na kampuni kubwa ya mavazi nchini Marekani ikimtaka aposti picha moja ya tangazo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na itamlipa dola laki 9. Kim amesema yeye aliona ni fedha nyingi lakini ilimpasa aombe ushauri kwa mumewe, lakini Kanye West akamkatalia kufanya hivyo. “ Nilimpigia kuomba ushauri lakini akaniambia..’No babe, I really don’t want you to do that,’ nilipomuuliza kwanini? akasema kama unanipenda achana na hilo tangazo, “amesema Kim kwenye mahojiano hayo. Hata hivyo, wiki mbele baadae May 12 mwaka huu siku ya Mama Dunia...

Video: Zee – Kidogo

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki kutoka Kwetu Studio, Zee ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Kidogo’.Video ya wimbo huo imeandaliwa na Kwetu Studio huku audio ikiandaliwa na Boom Tune Production.

Utaipenda cover ya wimbo ‘Madam Hero’ alivyopita nayo msanii chipukizi, Fany(Video)

Image
NancyTheDreamtz Wasanii chipukizi wa muziki wa BongoFleva, Fany ameamua kufanya cover ya wimbo Madam Hero ulioimbwa na mwanadada, Hamisa Mobetto. Hebu sikiliza kwa makini halafu na wewe utoe maoni yako juu ya kile alichokifanya. Related Articles

Wema Sepetu ataja sababu za kufanya Movie yake na wasanii wa Ghana bila kumshirikisha msanii yeyote wa Kitanzania (Video)

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa Bongo movie pia aliyekuwa miss Tanzania 2006 Wema Sepetu amefunguka mwanzo mwisho kuhusu sanaa nzima ya Bongo movie. Msanii aliongea hayo wakati anaongea na waandishi wa habari juu ya movie yake ya D.A.D ambaye aliamua kwenda kuifanyia nchini Ghana na msanii kutoka nchini humo ambaye ni Van Vicker. Wema alisema ” Niliamua kwenda kufanya muvi huko ili kubadilisha mazingira kidogo ya uigizaji kwani kama movie za Kitanzania na Kiswahili tulishafanya sana” aliongeza “Mimi ndio niliyemtafuta Van Vicker ili tufanye kazi lakini pia nilimwambia atafute waigizaji yeye mwenyewe anaona wanafaa”

Jeshi la Uganda lazindua kondomu zenye kibwagizo ‘Usiende nyama kwa nyama’ kuwalinda wanajeshi wake

Image
NancyTheDreamtz Jeshi la Uganda limezindua mifuko ya kondomu katika kambi yake ya kijeshi ya UPDF Bombo iliyopewa kibwagizo cha usiende nyama kwa nyama.  Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Brigedia Leopoldo Kyanda amesema mwanajeshi hawezi kutekeleza wajibu wake ipasavyo bila wenyewe kujilinda kutokana na maambukizi ya zinaa na hususan virusi vya ukimwi. Kondomu hizo zimepewa jina Ulinzi na zinatarajiwa kusaidia katika juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vinavyosababisha Ukimwi. Kitengo cha kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi jeshini kilizindua nembo hiyo mpya kwa ushirikiano na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali.