Posts

Showing posts from March 4, 2020

Senegal na Tunisia Zathibitisha kuwa na waathirika wa corona

Image
NancyTheDreamtz Senegal na Tunisia zimethibitisha kuwa na waathirika wa corona.  Waziri wa afya wa Senegal Bw. Abdoulaye Diouf Sarr amesema mgonjwa aliyeambukiziwa ni raia wa Ufaransa, baba wa watoto wawili, alirudi Dakar mnamo tarehe 26 mwezi Februari kutoka Paris kwa ndege ya Senegal, baada ya safari ya mapumziko kusini mwa Ufaransa. Tarehe 28 mwezi Februari, idara ya afya ya Ufaransa iliarifiwa na zahanati binafsi kuwa mtu mmoja alionyesha dalili za COVID-19, baadaye alithibitishwa kuambukizwa COVID-19 katika Taasisi ya Pasteur mjini Dakar, lakini hali yake sio mbaya, na familia yake imewekwa kwenye karantini. Waziri huyo amewataka raia wasichanganyikiwe, na kuchukua hatua za kujikinga zinazotangazwa na wizara ya afya.     Mgonjwa aliyebainika Tunisia ni Raia wa Tunisia ambaye ametokea Italy. Nchi zenye Watu wenye virusi hivyo kwa Afrika zimefikia tano, nyingine ni Algeria,Misri na Nigeria

Vijana 11 Wakamatwa Kwa Utapeli wa Ile PESA Tuma Kwenye Number Hii

Image
NancyTheDreamtz Jeshi la Polisi linawashikilia vijana 11 wenye umri wa kati ya miaka 20 - 25 kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi kupitia Mtandao wa Facebook kwa kutumia majina ya viongozi wa Serikali na Wasanii maarufu Wanadaiwa kuwa walikuwa wakishirikiana na Mawakala wa kusajili laini za simu kupata laini zilizosajiliwa kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzitumia kutapeli watu kwa kuwatumia jumbe fupi za simu zinazosema 'Ile pesa tuma kwenye namba hii' Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema vijana hao walifungua akaunti Facebook zenye majina ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo -

Meneja wa GRAMMY Ashangazwa na Uwezo Pamoja na Uthubutu wa Diamond Platnumz

Image
NancyTheDreamtz Moja ya mameneja wa muziki duniani na mfanyakazi anayefanya kazi kwenye ofisi za waandaji tuzo za Grammy @marlonfuentes ameshangazwa na uwezo wa Diamond Platnumz baadabya kuudhuria kwenye show ya Diamond iliyofanyika kwenye Los angels Marekani Kabla ya kuudhuria show hiyo meneja huyo alitembelewa ofisini kwake na Diamond Platnumz akiwa na uongozi wake na kuzungumza mambo mawili matatu kuhusu muziki. Meneja huyo ameahidi kuwa kuna uwezekano mkubwa kumuona Diamond kwenye tuzo za Grammy hivi karibuni HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG < DOWNLOAD HAPA > Meneja huyo ameonesha kufurahishwa na uwezo wa Diamond katika kuwapa mashabiki kile wanataka na amemwita 'Mmoja wa wasanii wakubwa duniani kutoka Tanzania'. MARLON alishawahi kuwa Dj wa mwanamuziki Shakira .

Rais Magufuli Akutana na Maalim Seif Sharif Hamad

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanasiasa Mkongwe na Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu Jijini Dar Kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao na baada ya kumaliza walisalimia kwa namna ambayo hawakugusana, awali walipungiana mikono kwa mbali na mwisho waligusanisha miguu Salamu hizo ni kutekeleza ushauri ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya Corona

CHADEMA yamgomea Membe kisa Lissu..Aende tu Vyama Vingine

Image
NancyTheDreamtz Baraza la Wazee CHADEMA wamesema hawafikilii Benard Membe atajiunga na chama hicho ila wengependa zaidi kuona anahamia vyama vingine vya upinzani kwani atawasaidia kuzigawa kura za Chama cha Mapinduzi CCM.

Kisa Tanasha DONA..Diamond Leo Kuongea na Waandishi wa Habari Serena Hotel

Image
NancyTheDreamtz From @diamondplatnumz: Kesho Panapomajaaliwa nitakuwa na zungumza na Ndugu zangu waandishi Pale SERENA HOTEL Muda wa saa nne asubuhi....Tafadhali Usikose Kufatilia🙏🏼