WAKATI akijiandaa kumfanyia sikukuu maalumu ya kuadhimisha kuzaliwa kwake mwanaye Tiffah, sherehe ya bethedai ya Dylan mtoto aliyezaa na Hamisa Mobeto aliyoifanya hivi karibuni jijini Dar imemponza mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kujikuta akinagwa mitandaoni mpaka basi, Risasi Jumamosi linakupasha. Matarajio ya sherehe ya Tiffah, mtoto aliyezaa na mrembo Zarina Hassan ‘Zari’ itakayofanyika Afrika Kusini Agosti 18 ni kufanya kufuru ambapo mambo yamepangwa kuwa moto na matamu kwa siku tatu mfululizo huku mamilioni ya fedha yamepangwa kutumika. Chanzo cha kunangwa kwa Diamond kilianzia kwenye posti aliyoiweka kwenye Istagram yake na kuandika maneno yafuatayo: “Very Happy Birthday to the Next Platnumz…My Kitinda Mimba, Mswahili Mwenzangu, Maskini Mwenzangu…Mnyonge Mwenzangu…” “Mengi Uloyapitia Ukiwa mdogo, usiyejua hili wala lile yamenifanya nikupende sana na kuhakikisha nakulinda na kukutunza kwa hali yoyote ntayojaaliwa…Insha Allah. “Mwenyez Mungu akuk...