Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 18, 2021 imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara Marijan Msofe (53) maarufu Papa Msofe na wenzake wanne. Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo akieleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao. Msofe na wenzake walikuwa wanakabiliwa wa mashtaka matano likiwemo la kujipatia Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu. Mbali na Papa Msofe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 124/2019 ni Wenceslaus Mtu(49), Mwesigwa Mhingo (36), Josephine Haule (38) na Fadhil Mganga (61). Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa hao umetolewa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Awali, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa DPP ameieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo. Baada ya upande mashtaka kueleza hiyo, Shai...