Posts

Showing posts from August 26, 2018

Kelvin John ‘Mbappe’ Kazitosa Simba, Yanga malengo yake ‘yakiutu-uzima’

Image
NancyTheDreamtz Kelvin John ‘Mbappe’ amekuwa gumzo sana kwenye timu ya taifa ya vijana wa U17 Serengeti Boys mshambuliaji anaevaa jezi namba 10. Inawezekana umemuona lakini hufahamu historia yake hadi kufika Serengeti Boys. Jina Kelvin Pius John mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ‘Serengeti Boys’, nina umri wa miaka 16 nipo kidato cha pili. Ni mtoto wa ngapi kwa mzee Pius John? Tupo wawili, kwa upande wa mama nipo pekeangu lakini kwa baba tupo wawili, mimi ndio mtoto wa kwanza. Form Two mwaka huu wana fanya mtihani wa taifa, anajigawa vipi shule na mpira? Nikiwa kambini kabla ya mashindano, kuna program naifanya kupitia laptop yangu. Natumiwa material ya shule na home work au vipindi vilivyoendelea darasani wakati mimi sipo mwalimu ananitumia kupitia email yangu nafanyia kazi. Natumiwa mitihani pia nafanya halafu namtumia tena mwalimu. Elimu ni kitu kikubwa, mpira una mwisho naweza kufika umri ambao huwezi tena kucheza mpira lakini ukiwa na elimu unaweza kufungua kampuni na kujie...