Usain Bolt kuitumikia klabu ya Central Coast Mariners

Mwanariadha anaeaminika kuwa na kasi zaidi duniani, Usain Bolt ametua jijini Sydney  nchini Australia asubuhi ya leo tayari kwaajili ya majaribio kabla ya kujiunga na klabu ya Central Coast Mariners.

Bolt amedhamiria kweli kutimiza ndoto zake katika mchezo wa soka baada ya kutua Sydney kukamilisha dili hilo ndani ya timu ya Central Coast Mariners inayoshiriki A-League ya nchini Australia.

Bingwa huyo mara nane wa michuano ya Olympic ameeleza hamu yake kuhamia upande wa soka mara baada ya kustaafu mchezo wa riadha na kusisitiza kuwa atabaki Australia kwa muda wake wote.
Raia huyo wa Jamaica mwenye umri wa miaka  31, tayari ameshafanya mazoezi ya soka na klabu kama Borussia Dortmund, Stromgodset na Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele