Rais wa Simba na Wenzake Kusomewa Maelezo Ya Awali Septemba 3

Rais wa Simba na Wenzake Kusomewa Maelezo Ya Awali Septemba 3
Kesi  ya kughushi na kutakatisha Dola za Marekani 300,000 inayomkabili Rais wa  Simba, Evance Aveva, na Makamu wake, Godfrey Nyange, imepangwa kusomwa maelezo ya awali Septemba 3, mwaka huu.

Jana, kesi ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi baada ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa mgonjwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Simba lakini hakuwapo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa siku saba ili upande wa Jamhuri utoe taarifa utawasomea lini washtakiwa maelezo ya awali.

"Mheshimiwa Hakimu tunaomba tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali kwa sababu tayari mahakama imeamuru hati ibadilishwe washtakiwa ambao hawajakamatwa waondolewe ili kesi iendelee," alidai Nkoko.

Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itasikilizwa maelezo ya awali Septemba 3.

Mapema, Mahakama hiyo ilikubali upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashtaka kutoka washtakiwa wawili na kuwaunganisha Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe na mfanyabiashara Franklin Lauwo.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwamo kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji dola hizo.

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)