Mashabiki wa Simba wapata ajali wakielekea Mwanza

Gari iliyokuwa imewabeba mashabiki wa Simba tawi la Ubungo Terminal limepata ajali baada ya kumgonga mwanamke mmoja mwendesha baiskeli kisha kuacha njia maeneo ya Nzega Ndogo.

Mashabiki hao walikuwa wakielekea jijini Mwanza kushuhudia mchezo wa ngao ya jamii baina ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mwanamke huyo amepata majeraha na kukimbizwa hospitali wakati hakuna abiria aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo licha ya kushindwa kuendelea na safari.
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wanatarajia kushuka uwanja wa CCM Kirumba hii leo kuwakabili mabingwa wa FA klabu ya Mtibwa kwenye mchezo wa Ngao ya jamii ikiwa ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele