Lulu amebadilika sana, amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu – Ray C

Muimbaji Ray C, amemzimikia mwigizaji wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa jinsi alivyoamua kushika dini zaidi kwa sasa.

Ray C amesema Lulu amemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua, kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.
“Aisee, nimemfuatilia sana Lulu tangu ameanza kupata matatizo ya kesi yake (ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya msanii Steven Kanumba) amebadirika sana. Sasa amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu,” alisema Ray C.
“Yaani nikiwa namwangalia picha zake au video zake mitandaoni anazoimba nyimbo za dini mpaka machozi yananilenga, hadi fikra zinakuja maana sikumbuki mara ya mwisho lini niliingia kanisani.
“Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali. Hakika nimejifunza kitu kutoka kwake, nawashauri watu wajirudi kwa kutubu kwa mwenyezi Mungu kutokana na makosa waliyofanya, wasisubiri hadi matatizo yawapate.”
Kumekuwa na video zinazosambaa mita ndaoni zikimwonyesha Lulu akiwa kanisani akicheza na waumini wenzake, haijajulikana nani msambazaji wa video hizo.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele