Simba yaipiga Mtibwa Sugar na kutwaa Ngao ya Jamii

Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa Ngao ya jamii uliyopigwa CCM Kirumba Mwanza.

Simba imepata mabao yake kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga dakika ya 29 na Hassan Dilunga 45+3 wakati bao pekee la Mtibwa Sugar likifungwa na Kelvin Kongwe 33.
Kukamilika kwa mchezo huo ni ishara sasa ya kufunguliwa rasmi kwa michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara inayorajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele