Bill Nass Ahamia kwa Mwana FA

Bill nass Ahamia kwa Mwana FA
Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'labda' amefunguka na kuweka wazi kwa jamii kuwa anatarajia kufanya mambo makubwa katika tasnia ya muziki, kwa kushirikiana na mkongwe Mwana Fa katika hilo.


Billnass amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuenea picha mtandaoni ikiwaonesha marapa hao wawili wakiwa pamoja katika hali fulani ya maongezi na kupelekea mashabiki zao mbalimbali kuwa na maswali mengi juu ya hilo.

"Kuna vitu vingi vikubwa kati yangu mimi na Mwana Fa, kimuziki na hata kwenye maisha mengine ya kawaida kama vile biashara na mambo mengine. Ninafanya hivyo kwasababu FA ni zaidi ya ndugu kwangu mimi ila kimuziki kuna kitu kikubwa sana kinakuja", amesema Billnass.

Mbali na hilo, Billnass amesema muziki kwa sasa umekuwa biashara nzuri ndio maana huwa wanachagua watu wa kufanya nao collabo, ambao wanaamini wataweza kuwafikisha mbali na sio kila msanii anafaa kufanya naye kazi.

Billnass ni miongoni mwa wasanii waliwahi kukiri hadharani kuwa hatarajii kuingia mkataba na kampuni yoyote kwa lengo la kuajiriwa kufanya kazi, kwa madai hatokuwa huru katika kufanya harakati zake za muziki na masuala mengine.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele