Wamiliki wa Blog ya Dauda.com waachiwa kwa dhamana Mahakama ya Kisutu

NancyTheDreamtz
Wamilikiwa wa blog ya Dauda.com  wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mkazi Kisutu ambao ni pamoja na mtangazaji wa Clouds fm Shaffih Dauda. Wawili hao wanatuhimiwa kwa kosa la kuendesha blogs bila kuwa na kibali.
Licha ya Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 mwezi wa kumi,washtakiwa hao walikataa tuhuma hizo za kumiliki blog bila kuwa na kibali.
Wakili wa upande wa Jamhuri ameiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kwa Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambone ameiomba Mahakama kuwapa dhamana wateja wake kwa kuwa haki ya kupata dhamana ipo na Hakimu wa kesi hiyo amekubali kuwapa dhamana washtakiwa hao.
Shafiih na wenzake ambaye anashikiliwa ni Ben Ali (Ben On Air) ambaye alikuwa muendeshaji wa Dauda TV kupitia mtandao wa (Youtube) walikamatwa wiki iliyopita kwa kosa la kuendesha blog hiyo bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele