Meli iliyopata ajali miaka 400 yapatikana, inadaiwa ilikuwa njiani kutoka India
NancyTheDreamtz
Wagunduzi hao waamini kwamba meli ilikuwa njiani kutoka India wakati ilipozama kati ya mwaka 1575 na 1625. Nyakati hizo zinakadiriwa kuwa ndiyo kilele cha biashara ya viungo kati ya Ureno na nchi za Asia.
Watafiti wa mambo ya kale wamegundua meli iliyopata ajali miaka 400 iliyopita karibu na pwani ya Ureno, katika tukio ambalo wataalam wameliita “ugunduzi muhimu”.
Kwa mujibu wa mtandao wa REUTERS, baadhi ya viungo, vyombo vya kauri na mizinga ikiwa na nembo ya Ureno vimetapakaa katika eneo la karibu na Cascais ambapo si mbali sana kutoka Mji Mkuu Lisbon.
Wagunduzi hao waamini kwamba meli ilikuwa njiani kutoka India wakati ilipozama kati ya mwaka 1575 na 1625. Nyakati hizo zinakadiriwa kuwa ndiyo kilele cha biashara ya viungo kati ya Ureno na nchi za Asia.
Inadhaniwa kuwa huu ni ugunduzi mkubwa kabisa ambao umechukua takribani miaka 10 kwa mujibu wa mkurugenzi wa zoezi hilo, Jorge Freire ambapo akisisitiza ni jambo muhimu zaidi kwa Ureno.
Comments