Simba Yaenda Kuweka Kambi Zanzibar Kwaajili ya Kupambana na Yanga

NancyTheDreamtz
Simba Yaenda Kuweka Kambi Zanzibar Kwaajili ya Kupambana na Yanga
Kikosi cha Simba kinaondoka leo jijini Dar es Salaam kuandaa dawa maalum ya kuwamaliza Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Septemba 30 Jumapili hii.

Simba wanaenda kuweka kambi hiyo Zanzibar kama ilivyo mara nyingi pindi wanapojiandaa kucheza na Yanga tayari kuja kukabiliana na watani zao wa jadi walio na alama 12 kileleni.

Kuelekea mchezo huo, wachezaji wa kikosi cha timu hiyo waliokuwa Dar es Salaam kwa ajili ya program maalum iliyokuwa chini  ya Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, wataungana na wenzao visiwani humo.

Wachezaji hao ambao miongoni mwao ni Haruna Niyonzima na Juuko Murushid wataongeza nguvu kwa ajili ya kujifua vilivyo kuelekea mechi hiyo.

Ikumbukwe Simba inaenda kucheza na Yanga ikiwa na kumbukukumbu ya ushindi katika mchezo wao wa mwisho kwa bao 1-0 msimu uliopita.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele