Skip to main content

Kwa jeuri hii ya fedha aliyoionesha Davido, angekuwa Bongo angepata tabu sana (+Audio)

NancyTheDreamtz
Msanii kutoka Nigeria, Davido jana ameonesha jeuri ya fedha kwa mara nyingine baada ya kuwanunulia members 18 wa 30 Billion Gang toleo jipya la simu za iPhone XS.
Davido kupitia Insta Story alionesha simu hizo na kusema kuwa amenunua kwa ajili ya watu wake wote wa 30 Billion Gang akiwemo mchumba wake, Chioma .
Toleo hilo la iPhone XS ndio toleo jipya la simu hizo pendwa duniani, na simu moja inauzwa dola $1,400 ambayo ni sawa na Tsh milioni 3.
Image result for iphone XS
Kwa hesabu ndogo Davido ametumia tsh milioni 54 kuwanunulia simu rafiki zake ambao wanaunda kundi hilo la 30 Billion Gang.
30 Bilion Gang ni kundi ambalo Davido ndio kiongozi lakini pia wapo binamu zake wawili Sina Rambo na B-Red na meneja wake Asa Asika.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake wameshusha maombi wakitaka nao wapewe zawadi za simu hiyo mpya  ya iPhone XS.
mrbrownchips@davidoofficial boss abeg bless me with phone…I saw the ones you got for your team…me na your team too abeg.
youngwiz_official@davidoofficial can I have one of the old iPhone X please don’t waste it.
stdave_williams_@davidoofficial please I saw you bought the latest iPhone for all 30billion gang member. please I’m waiting for mine here in Accra Ghana. I dey fight for you here, so we need to keep the movement upgraded.
Usumbufu anaoupata Davido wa kuombwa simu nchini Nigeria, bila shaka hata kama angekuwa Tanzania angeupata tu kwani nani asiyependa kutumia iPhone XS simu bora zaidi kwa sasa duniani.

Related Articles

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele