Mizigo ya Waliofariki na Majeruhi Yaanza Kuibuka

NancyTheDreamtz

Mizigo zaidi inasukumwa ufukweni kutoka ndani ya kivuko cha Mv Nyerere baada ya wataalam kufanikiwa kukinyanyua na kukilaza ubavu 

Ukara. Baadhi ya mizigo ikiwamo mikungu ya ndizi, mikoba na majamvi  iliyokuwa ndani ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozana ziwa Victoroa imeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Hali hiyo imejitokeza baada ya wataalam wa uokoaji kufanikiwa kikilaza ubavu kivuko hicho hicho kilichopinduka Septemba 20 na kujifunika kifudifudi.

Kazi ya kunyanyua kivuko hicho inafanywa na wataalam kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wakishirikiana na maofisa kutoka kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza.

Operesheni ya uokoaji tayari imefanikisha kuopoa miili ya watu 227 waliokufa katika ajali hiyo, huku wengine 41 wakiokolewa hai.

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)