Afya ya Haji Manara yatetereka, mwenyewe adai amelishwa sumu na sio presha ya matokeo ya Simba

NancyTheDreamtz
Baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameshikwa na presha iliyopelekea kulazwa mkoani Shinyanga, hatimaye mwenyewe aweka wazi kinachomsumbua.
Haji Manara
Manara amesema kuwa alikula chakula chenye sumu, na ndio sababu iliyompelekea kulazwa na sio presha ya matokeo mabaya ya klabu yake kama inavyoandikwa mitandaoni.
Siumwi pressure wala moyo kama inavyoandikwa mitandaoni..nahic nimepata food poisoning na niwashukuru Madaktari walionihudumia awali Shinyanga na Mwanza ..now nisharejea Dar teyari kwa vipimo zaidi…Insha’Allah kila kitu kitazidi kuwa salama,“ameeleza Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Klabu ya Simba imekuwa na matokeo mabovu kwa msimu huu ambapo wiki iliyopita imepokea kichapo cha goli 1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele