Sitaki kuolewa tena na kijana, nataka mwanaume mzungu aliyeachika – Hamisa Mobetto

NancyTheDreamtz
Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka wazi mwanaume ambaye anataka kuishi naye kwa sasa, ambapo amedai kuwa anataka mwanaume wa kizungu ambaye alishawahi kuachika na mwenye watoto.
Hamisa Mobetto
Akizungumzia vigezo vya mwanaume anayemtaka, Hamisa amesema kuwa kwa sasa hapendi kuolewa na vijana na anatafuta Mzungu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 45.
Mimi hapa nataka labda mzungu au mtu mzima,  awe alishawaki kuachwa au Mgane kwa hiyo ndio hivyo, yaani nikisema kijana dah hapana. Awe angalau miaka 45 kwa sababu mimi mwenyewe nina watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wangu,“amesema Hamisa Mobetto kupitia EATV.
Hamisa Mobetto tayari ameshazaa watoto wawili na wanaume wawili tofauti tofauti, ambao ni Diamond Platnumz na Majizzo na amesema kwa sasa hawezi kurudiana na yeyote kati yao.
Kwa upande mwingine, Hamisa Mobetto amekiri kuwa sauti iliyosambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita akiongea na Mganga wa kienyeji ilikuwa ni ya kwake.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele