Posts

Showing posts from November, 2018

Kasi ya Kagere Yamuibua Hamissi Tambwe "Kagere ni Moto wa Kuotea Mbali Sitashangaa Akiwa Mchezaji Bora Msimu Huu"

Image
NancyTheDreamtz Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, ameibuka na kusema straika wa Simba, Meddie Kagere ni moto wa kuotea mbali. Ni baada ya Kagere kufunga mabao yote mawili juzi, wakati Simba ikiichinja JKT Tanzania 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Tambwe amesema amekuwa akimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo ambaye alijiunga na Simba Juni, mwaka huu akitokea Gor Mahia ya Kenya. Tambwe amempongeza Kagere kwa kufikia rekodi yake ya kufunga mabao saba katika mechi 11 za kwanza Simba. Alisema, yeye pia msimu wa 2013/14 aliposajiliwa na Simba akitokea Vital’O ya Burundi, alifunga mabao saba katika mechi 11 za kwanza. “Kwa hiyo, Kagere ni mmoja kati ya washambuliaji hatari sana msimu huu na jinsi mambo yanavyoenda, sitashangaa kama ataibuka mfungaji bora. “Ana tofauti kubwa na washambuliaji wengine wa Simba, anafunga Uwanja wa Taifa lakini pia katika viwanja vya mikoani, kwa hiyo nampongeza kwa hilo, lakini pia kitendo chake cha kuifikia rekodi yang

Daimond Amuomba Alikiba Kuungana naye Kwenye Tamasha Lake la Wasafi Festival

Image
NancyTheDreamtz MKURUGENZI wa Wasafi Media, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemuomba msanii mwenzake, Alikiba,  kuungana naye kwenye Tamasha la Muziki lililoandaliwa na uongozi wa Wasafi ili kuonyesha kwamba wasanii wa Tanzania wanaweza kufanya matamasha makubwa kama yanayofanywa kwenye mataifa makubwa kama Marekani, Canada na Uingereza. Diamond amesema hayo leo Jumatatu, Novemba 5, 2018 wakati akizindua tamasha hilo na Urushaji wa Matangazo wa Kituo cha Redio cha Wasafi FM katika ofisi za Wasafi media zilizopo, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. “WASAFI FESTIVAL ni tamasha la kwetu wote, tunataka tujitahidi sana kuhakikisha msanii yeyote ambaye atakua tayari kushirikiana na sisi, tutashirikiana naye, tutafurahi sana kwenye Wasafi Festival endapo tukiwa na mtu kama Alikiba, kwa sababu ni tamasha la nyumbanui, ni matamasha yetu. “Lengo letu ni kuonyesha watu wa nje kuwa muziki wa Tanzania ni mkubwa kwelikweli, ndicho tunachotaka kukifanya, hata kama mtu akitoka Ulaya, Marekani au Ni

Kidato Cha NNE Kuanza Mitihani Leo....Serikali Yatoa Onyo Kwa Watakaoiba Mitihani

Image
NancyTheDreamtz Mtihani  wa taifa wa kidato cha nne unaanza leo, huku Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) likitoa onyo kali kwa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu. Baraza hilo limesisitiza kuwa halitasita kukifutia matokeo kituo chochote cha mtihani ambacho kitabainika kujihusisha na udanganyifu. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mtihani huo ambao utawahusisha jumla ya watahiniwa 427,181. Dk. Msonde alisema baraza linazitaka kamati za mitihani za mkoa, halmashauri kuhakikisha kuwa taratibu zote za uendeshaji mitihani ya taifa zinazingatiwa ipasavyo. “Kamati zihakikishe kuwa mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha kutokea kwa udanganyifu,” alisema. Alisema wasimamizi wote wanatakiwa kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu. Wasimamizi wanaaswa kujiepusha na vitendo vya

Matokeo ya Uchaguzi wa Simba SC

Image
NancyTheDreamtz Club ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumapili ya November 4 2018 ilifanya mkutano wake mkuu sambamba na uchaguzi mkuu wa mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Simba SC ambapo kura zilihesabiwa hadi alfajiri ya November 5 2018. Simba SC sasa inahesabika kama kampuni baada ya kufanikiwa kuingia katika mfumo wa mabadiliko ya uwekezaji wa hisa, ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji ndio alishinda Zabuni ya uwekezaji ndani ya club ya Simba hivyo maamuzi ya timu hiyo kwa sasa yatakuwa yanajadiliwa ndani ya bodi.

Breaking News: Mahakama Yamwachia Huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo

Image
NancyTheDreamtz Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo leo Novemba, 5  baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha makosa mawili yaliyokuwa yanamkabili Nondo alikuwa anakabiliwa  na mashtaka mawili; shitaka la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa ametekwa na kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Kimewaka tena: Marekani Yaiwekea Vikwako Iran....Jeshi La Iran leo Kufanya Mazoezi Makubwa Kuonesha Ubabe Wao

Image
NancyTheDreamtz Marekani imetangaza kuwa leo Nov 5 imeirejeshea vikwazo nchi ya Iran vitakavyolenga sekta ya mafuta na sekta ya kifedha. Marekani imesema imeiwekea Iran vikwazo vigumu zaidi ambavyo haijawahi kuiwekea. Vikwazo hivyo vitalenga mauzo ya mafuta, usafiri kwa njia ya baharini na mabenki ambavyo vyote ni muhimu sana kwa uchumi. Maelfu ya raia wa Iran wakiwa na mabango yaliyoandikwa  "Kifo kwa Marekani" wameandamana  wakiitaka serikali  yao kutofanya mazungumzo yoyote na Marekani. Jeshi la Iran nalo limesema kuwa litafanya mazoezi ya kijeshi leo Jumatatu na Jumanne kuonyesha uwezo wake wa kijeshi. Marekani imetangaza vikwazo hivyo  baada ya  Rais Trump kutangaza  kujitoa kwenye  mkataba wa mwaka 2015 uliolenga kupunguza mipango ya nyuklia ya Iran. Marekani inasema inataka kuzima vitendo viovu vya Ina vikiwemo udukuzi wa mitandao, majaribio ya makombora ya masafa marefu na uungaji mkono wa makundi ya kigaidi mashariki ya kati. Zaidi ya watu 700

RC Makonda Afunguka Siri Ya Kumwaga Machozi Kanisani...."Watu Wanadhani ni Utani, Ila Mbinguni Wanajua"

Image
NancyTheDreamtz Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutokwa na machozi akiwa katika ibada katika kanisa la Efatha linaloongozwa na mtumishi wa Mungu Josephat Mwingira kiongozi huyo ameibuka na kutoa neno. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Makonda amechapisha video ambayo alionekana  anatokwa na machozi kanisani hapo na kuandika ujumbe ambao alibainisha watu wengi hawajui kilichotokea. Makonda ameandika;  “Powerful, very powerful watu hawaelewi nini kimefanyika Ila mbinguni wameelewa na wameandika, people think it’s a joke. Ila kwa Mungu hakuna mzaha, asante Mungu Kwa kusimama upande wangu” Hivi karibuni Mkuu wa huyo wa Mkoa Dar es salaam alianzisha kampeni maalum ya kuwakamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, na kuunda kamati maalum ya watu 17 ili ya kushughulika na suala hilo. Jana kupitia ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje,  serikali ilisema zoezi linaloendeshwa na Mkonda  ni mawazo yake binafsi na si msimamo wa serikali.

Diamond Azindua Rasmi Wasafi Festival na Wasafi FM

Image
NancyTheDreamtz Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB) leo imezindua kituo cha redio cha Wasafi FM pamoja na tamasha la Wasafi litakalofanyika katika maeneo mbalimbali nchini. Mkurugenzi wa WCB, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' amesema uzinduzi wa redio hiyo unalenga kutoa fursa kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla kusikika. "Siku ya leo redio yetu ya Wasafi FM itaanza kusikika kupitia masafa ya 88.9 katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Bado ndio tupo kwenye majaribio kwani mambo mazuri yanakuja na tumefanya hivi kwa sababu hata sisi wenyewe tulifanikiwa kwa sababu tulisapotiwa na vyombo vya habari," alisema Diamond. Kuhusu Tamasha la Wasafi, Diamond alisema mbali ya kuburudisha, watafanya huduma za kijamii na kutangaza utalii. "Licha kufanya tamasha, sisi tungependa kuonyesha kitu cha tofauti. Tutajitahidi katika kila mkoa tunaoenda kurudisha kwa jamii kile ambacho tunakipata kutoka kwao. Tutaangalia changamoto ya eneo husika kama itakuwa n

VIDEO: Diamond amfanyia surprise Dudu Baya uzinduzi wa Wasafi Festival ‘kuna wasanii hawapewi nafasi kisa hawatoi nyimbo’

NancyTheDreamtz Msanii wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz amemfanyia saplaizi Dudu Baya kwa kumtaja kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye taamasha la Wasafi Festival 2018. Akiongea na Waandishi wa Habari leo Novemba 05, 2018 jijini Dar Es Salaam kwenye uzinduzi wa Tamasha la Wasafi Festival 2018, Diamond amesema kuwa kuna wasanii wengi wakubwa huwa hawapewi nafasi ya kutumbuiza kwenye majukwaa makubwa kwa kisingizio kuwa hawajatoa nyimbo mpya. “ Kaka yetu Dudu Baya muda mrefu watu hawajamuona kwenye show ya steji, sasa nawambia kwamba nitafurahi sana akiwepo kwenye show ya Wasafi Festival. Unajua sio tu Dudu Baya peke yake unajua kuna wasanii wengi wana sauti kubwa lakini sometimes hawapewi nafasi kwenye matamasha kwa sababu tu hawajatoa wimbo mwaka huu lakini kuna watu wanawapenda. “amefunguka Diamond Platnumz na kusisitiza. “ so wanaoandaa Wasafi Festival nitaongea nao na Dudu Baya pia wamuweke kwenye tamasha, nitafurahi kwa sababu nilikuwa tu namuonag

CHOMBO KWA HEWA: Wasafi FM yaanza kusisikika Dar Es Salaam, ni muziki kwenda mbele

Image
NancyTheDreamtz Kama upo Dar Es Salaam na ume-Tune Frequency za 88.9 FM na unasikiliza mixing za hatari basi jua kuwa hiyo ni redio mpya hapa mjini ya Wasafi FM. Hata hivyo, ishu imesanukiwa na wadau tu, kwani Mkurugenzi mwenyewe Diamond Platnumz hajazungumza chochote kuhusu mitambo hiyo kuwashwa. Mwanzoni mwa mwezi huu, Diamond ali-tweet kwa kuandika “ Naombeni ruksa niwashe Wasafi FM “.

Yanga kuweka hadharani mchakato wa Uchaguzi Leo

Image
NancyTheDreamtz Wakati klabu ya Simba ikielekea kufanya Uchaguzi wake mkuu Novemba 4 2018, Uongozi wa Yanga nao umetangaza kuweka hadharani mchakato wa Uchaguzi wao leo. Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu, Omar Kaya, ameeleza kuwa uongozi utaeleza kila kitu kuhusiana na uchaguzi utakaofanyika kama utakuwa ni Mkuu ama wa kujaza nafasi. Kaya ameeleza hivyo kutokana na matamko tofauti tofauti ya klabu hiyo siku zilizopita kusema watafanya uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo zipo wazi baada ya viongozi kadhaa kujiuzulu. Viongozi kadhaa akiwemo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, pia aliyekuwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa, waliachia ngazi na nafasi zao zikiendelea kuwa wazi mpaka sasa. Mbali na nyadhifa hizo zilizo wazi, Yanga pia ilitoa matamko ya kueleza nafasi ya Mwenyekiti wao Yusuf Manji, itaendelea kuwepo kufuatia mkutano mkuu wa mwisho uliofanyika Juni 6 2018 kuamua Manji aendelee kukalia kiti hicho.

FIFA Yamfungia Maisha Rais wa Chama cha Soka Ghana

Image
NancyTheDreamtz Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo Alhamisi ya November 1 2018 zimeripotiwa taarifa za kumfungia rasmi maisha kujihusisha na soka aliyekuwa Rais wa chama cha soka Ghana Kwesi Nyantakyi. FIFA imetangaza kufikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa Kwesi alitenda kosa la kupokea rushwa kinyume na taratibu za kazi yake kutoka kwa muandishi wa habari za uchunguzi. Kwesi amekutwa na hatia ya kuokea rushwa ya zaidi ya Tsh Milioni 149 kutoka kwa mwanahabaribari aliyekuwa anafanya habari za uchunguzi wa ufisadi na rushwa katika mchezo wa soka.

Polisi Wapekua Nyumbani kwa Zitto Kabwe

Image
NancyTheDreamtz Polisi wamefanya upekuzi nyumbani kwa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe  na kumrudisha katika kituo cha Oysterbay kutoka Kituo Kikuu Wakili wa Mbunge Huyo Jebra Kambole amesema polisi wamefika nyumbani kwa mteja wake Maeneo ya Masaki Jijini Dar es Salaam na Kufanya upekuzi. Kambole ameeleza kuwa baada ya kukamatwa alipelekwa oysterbey polisi ambapo baadaye alihamishiwa kituo kikubwa cha polisi na hakulala hapo alihamishiwa kituo cha mburahati.

Kagere Afunguka Kuhusu Mabao Anayofunga Okwi

Image
NancyTheDreamtz Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda, amemfungukia mshambuliaji mwenzake Emmanuel Okwi na kusema kuwa anafurahi kuona anafunga. Okwi kwa sasa ana mabao 7 kwenye ligi akiwa nafasi ya pili mbele ya Eliud Ambokile mwenye mabao 8 huku Kagere akiwa na mabao matano. "Nimefurahi kuona Okwi anaendelea kufunga kwani sisi wote ni washambuliaji wa Simba, tuna jukumu moja la kuisaidia timu ifanye vyema hivyo  yeye akifunga na mimi nitafunga ni jambo jema ambapo inatusaidia sisi kutwaa ubingwa msimu huu, mimi sina shida," alisema. Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 23 Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Lipuli FC, wamefikisha pointi 25 huku vinara wakiwa ni Azam FC wenye pointi 27.

Breaking News: Wema Sepetu Asomewa Mashtaka ya Kusambaza Video ya Ngono Aachiwa kwa Dhamana

Image
NancyTheDreamtz MSANII wa Filamu nchini, Wema Sepetu leo Novemba 1, 2018 amepandishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisitu akikabiliwa na shtaka la kusambaza video yake isiyo na maadili (video za ngono) kupitia mitandao ya kijamii (Instagram). Wema amesomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Saanane Kasonde ambapo amekana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Tsh. Milioni 10 baada ya kupata mdhamini, Salim Limu ammbaye amekamilisha taratibu za dhamana hiyo. Aidha, Wema ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wake, Reuben Simwanza ametakiwa asiposti video/picha yoyote isiyo na maadili au inayoashiria ngono kwenye mitandao yake na kesi hiyo ikiahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu. Akizunngumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TCRA, Joannes Karungura amesema; “TCRA tupo makini, tunapenda kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na picha na video za hamna hiyo wazifute katika simu zao, kwa sababu hairuhusiwi wala kuposti kokote kuanzia sasa na kuendel

Chris Brown Aweka Mambo Sawa na Mzazi Mwenzie Kuhusu Matunzo ya Mtoto

Image
NancyTheDreamtz Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Chris Brown pamoja na mzazi mwenza Nia Guzman kuwa wako sawa kwa sasa kwenye suala zima la utoaji matunzo kwa mtoto wao Royalty baada ya kupelekana mahakamani miezi kadhaa iliyopita. Inaelezwa kuwa Chris Brown yupo mbioni kumnunulia Nia Guzman nyumba mpya atakayokuwa akiishi na mtoto wao Royalty mwenye umri wa miaka minne pamoja na kulipa kiasi cha zaidi ya Tsh Bilioni 2 kwaajili ya mwanasheria wa Nia Guzman. Miezi kadhaa iliyopita Nia Guzman aliiambia Mahakama kuwa alitaka kiasi cha zaidi ya Tshs Millioni 48 kila mwezi kwaajili ya matumizi ingawa Chris Brown alikua akitoa Tsh Millioni 5 kila mwezi, Inadaiwa kuwa wawili hao wapo katika harakati za kufuta mashtaka yanayowakabili Mahakamani baada ya miezi kadhaa kupita kuonekana kwa Chris Brown na Nia Guzman kuwa katika hali ya kuelewana kwaajili ya mtoto wao.

Magufuli Ataja Fedha za Ndege Zilipotoka

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema serikali imeweza kununua ndege kwa mara moja ni kutokana na fedha ambazo zimetokana na serikali kuwabana mafisadi. Akizungumza wakati wa uchangiaji kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake ambapo alitaja chanzo cha fedha hizo. “Mengine tumenunua ndege, kwa sababu watalii wetu walikuwa wachache, huwezi ukategemea shirika la ndege la jirani kuleta watalii kwenye nchi yako, tumeamua na ndio maana tumenunua ndege saba, hatukukopa nchi yoyote”, amesema Rais Magufuli “Ni hizi hizi fedha tulizowabana mafisadi ndio tumenunua ndege, unambana fisadi anaendelea kulia kule lakini fedha unepeleka kwenye ndege wananchi wengine wananufaika, na ukilipa kwa mkupuo gharama inakuwa ndogo”, ameongeza. Aidha Rais Magufuli kwa kipindi cha miaka mitatu serikali imefanikiwa kushughulikia masuala mbalimbali, ikiwemo utoaji wa elimu bure, na kuimarisha hali ya u

Yanga Yafunguka Kuhusu Mchezaji wao Ibrahim Ajibu

Image
NancyTheDreamtz Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuwa huenda nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu amegoma kucheza kwasababu ya kutolipwa mshahara, hatimae klabu ya Yanga imethibitisha kuwa nyota wake amerejea mazoezini baada ya kupona kutokana na majeraha. Yanga ambayo ilitoa mapumziko kwa wachezaji wake baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Lipuli FC imethibitisha kuwa leo wamchezaji wamerejea mazoezini na moja ya wachezaji walioanza mazoezi leo ni Ibrahim Ajibu na. ''Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi kimerejea mazoezini tayari kwa mchezo wa jumapili dhidi ya Ndanda Fc. Mchezaji Ibrahim Ajibu amerejea kikosini na amefanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wa Ndanda FC'', imeeleza taarifa ya Yanga. Ajibu hajaonekana uwanjani kwenye michezo miwili ya Yanga kati ya KMC na Lipuli FC ambapo mchezo wake wa mwisho kucheza ilikuwa ni dhidi ya Alliance FC, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Baada ya mchezo huo Yanga ilitoa taarifa kuwa Ajibu alikuwa akisumbuliw

Mbowe Apelekwa Nje ya Nchi kwa Matibabu

Image
NancyTheDreamtz Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Akiieleza mahakama mdhamini wa mbowe amedaiwa kuwa ameelezwa na mke wa Mbowe kuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na shinikizo la damu. Kufuatia maelezo hayo wakili wa serikali ameiomba mahakama kutoa amri ya kumkamata mbowe ili ajieleze kwa nini dhamana aliyopewa na mahakama kwanini isifutwe kwa kushindwa kufika mahakamani

Rais Magufuli: Nilifunga Ndoa Bila Koti la Suti, Mke Wangu Bila Gauni la Bi Harusi nilikunywa Pepsi ye Alikunywa Milinda

Image
NancyTheDreamtz Rais wa Tanzania John Magufuli leo amesema alifunga ndoa bila kuvaa koti la suti na mkewe Janeth hakuvaa gauni la bibi harusi. Ndoa hiyo ilifungwa wakati Magufuli akiwa mwanafunzi katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na haikuambatana na sherehe yoyote. Akiongea leo katika mdahalo uliofanyika UDSM kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake wan chi, Magufuli amesema amefurahi kurudi chuoni hapo ambapo si tu alipata elimu yake ya juu bali kufunga pingu za maisha. "Siku niliyooa watu wengi hawakujua…na haimaanishi sikuwa na pesa ya kununua koti au gauni la harusi kwa mke wangu, sikuona kama vitu hivyo ni vya msingi sana." "Tulienda hapo kanisani pete tukanunuliwa na Padre, tena zilikuwa za shaba. Padre pia alitununulia soda, nakumbuka mimi nilikunya pepsi na mke wangu alikunya mirinda...Baada ya hapo nikaendelea na shughuli zangu." Padre ambaye aliwafungisha ndoa hiyo na kutoa ufadhili wa pete na soda kwamujibu wa Rais Magufuli anaitwa M