Kagere Afunguka Kuhusu Mabao Anayofunga Okwi

NancyTheDreamtz
Kagere Afunguka Kuhusu Mabao Anayofunga Okwi
Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda, amemfungukia mshambuliaji mwenzake Emmanuel Okwi na kusema kuwa anafurahi kuona anafunga.

Okwi kwa sasa ana mabao 7 kwenye ligi akiwa nafasi ya pili mbele ya Eliud Ambokile mwenye mabao 8 huku Kagere akiwa na mabao matano.

"Nimefurahi kuona Okwi anaendelea kufunga kwani sisi wote ni washambuliaji wa Simba, tuna jukumu moja la kuisaidia timu ifanye vyema hivyo  yeye akifunga na mimi nitafunga ni jambo jema ambapo inatusaidia sisi kutwaa ubingwa msimu huu, mimi sina shida," alisema.

Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 23 Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Lipuli FC, wamefikisha pointi 25 huku vinara wakiwa ni Azam FC wenye pointi 27.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele