Daimond Amuomba Alikiba Kuungana naye Kwenye Tamasha Lake la Wasafi Festival

NancyTheDreamtz
Daimond Amuomba Alikiba Kuungana naye Kwenye Tamasha Lake la Wasafi Festival
MKURUGENZI wa Wasafi Media, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemuomba msanii mwenzake, Alikiba,  kuungana naye kwenye Tamasha la Muziki lililoandaliwa na uongozi wa Wasafi ili kuonyesha kwamba wasanii wa Tanzania wanaweza kufanya matamasha makubwa kama yanayofanywa kwenye mataifa makubwa kama Marekani, Canada na Uingereza.

Diamond amesema hayo leo Jumatatu, Novemba 5, 2018 wakati akizindua tamasha hilo na Urushaji wa Matangazo wa Kituo cha Redio cha Wasafi FM katika ofisi za Wasafi media zilizopo, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.


“WASAFI FESTIVAL ni tamasha la kwetu wote, tunataka tujitahidi sana kuhakikisha msanii yeyote ambaye atakua tayari kushirikiana na sisi, tutashirikiana naye, tutafurahi sana kwenye Wasafi Festival endapo tukiwa na mtu kama Alikiba, kwa sababu ni tamasha la nyumbanui, ni matamasha yetu.



“Lengo letu ni kuonyesha watu wa nje kuwa muziki wa Tanzania ni mkubwa kwelikweli, ndicho tunachotaka kukifanya, hata kama mtu akitoka Ulaya, Marekani au Nigeria waone kwamba Watanzania wako vizuri, kwa hiyo katika moja ya shoo, kaka yangu Alikiba akiwepo nitafurahi kwelikwli,” alisema Diamond.



Diamond amesema Wasafi Festival ni tamasha ambalo litawakusanya wasanii wote bila ubaguzi, litazunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania nzima kuanzia Mtwara, Iringa na Morogoro na mikoa mingine


Aidha, Diamond amesema katika tamasha hilo kutafanyika shindano la kusaka kusaka vipaji vya kuimba na kufanya mambo mbalimbali ya kijamii ili kurudisha fadhila zetu kwa jamii na mashabiki wa WCB.



Akizungumzia uzinduzi wa Wasafi FM, Diamond amesema kwa mara ya kwanza itakuwa ikisikika kwenye maeneo  ya Jiji la Dar es Salaam na  jirani katika masafa ya 88.9 na baadaye mikoa mingine itafuata.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele