Kasi ya Kagere Yamuibua Hamissi Tambwe "Kagere ni Moto wa Kuotea Mbali Sitashangaa Akiwa Mchezaji Bora Msimu Huu"

NancyTheDreamtz
Kasi ya Kagere Yamuibua Hamissi Tambwe "Kagere ni Moto wa Kuotea Mbali Sitashangaa Akiwa Mchezaji Bora Msimu Huu"
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, ameibuka na kusema straika wa Simba, Meddie Kagere ni moto wa kuotea mbali.

Ni baada ya Kagere kufunga mabao yote mawili juzi, wakati Simba ikiichinja JKT Tanzania 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Tambwe amesema amekuwa akimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo ambaye alijiunga na Simba Juni, mwaka huu akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Tambwe amempongeza Kagere kwa kufikia rekodi yake ya kufunga mabao saba katika mechi 11 za kwanza Simba.



Alisema, yeye pia msimu wa 2013/14 aliposajiliwa na Simba akitokea Vital’O ya Burundi, alifunga mabao saba katika mechi 11 za kwanza.

“Kwa hiyo, Kagere ni mmoja kati ya washambuliaji hatari sana msimu huu na jinsi mambo yanavyoenda, sitashangaa kama ataibuka mfungaji bora.


“Ana tofauti kubwa na washambuliaji wengine wa Simba, anafunga Uwanja wa Taifa lakini pia katika viwanja vya mikoani, kwa hiyo nampongeza kwa hilo, lakini pia kitendo chake cha kuifikia rekodi yangu ya kufunga mabao saba katika mechi 11 za ligi kuu,” alisema Tambwe ambaye msimu huo wa 2013/14 ndiye aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu baada ya kufunga mabao 19.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele