Breaking News: Wema Sepetu Asomewa Mashtaka ya Kusambaza Video ya Ngono Aachiwa kwa Dhamana
NancyTheDreamtz
MSANII wa Filamu nchini, Wema Sepetu leo Novemba 1, 2018 amepandishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisitu akikabiliwa na shtaka la kusambaza video yake isiyo na maadili (video za ngono) kupitia mitandao ya kijamii (Instagram).
Wema amesomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Saanane Kasonde ambapo amekana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Tsh. Milioni 10 baada ya kupata mdhamini, Salim Limu ammbaye amekamilisha taratibu za dhamana hiyo.
Aidha, Wema ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wake, Reuben Simwanza ametakiwa asiposti video/picha yoyote isiyo na maadili au inayoashiria ngono kwenye mitandao yake na kesi hiyo ikiahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu.
Akizunngumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TCRA, Joannes Karungura amesema; “TCRA tupo makini, tunapenda kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na picha na video za hamna hiyo wazifute katika simu zao, kwa sababu hairuhusiwi wala kuposti kokote kuanzia sasa na kuendelea.”

Comments