VIDEO: Diamond amfanyia surprise Dudu Baya uzinduzi wa Wasafi Festival ‘kuna wasanii hawapewi nafasi kisa hawatoi nyimbo’

NancyTheDreamtz
Msanii wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz amemfanyia saplaizi Dudu Baya kwa kumtaja kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye taamasha la Wasafi Festival 2018.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Novemba 05, 2018 jijini Dar Es Salaam kwenye uzinduzi wa Tamasha la Wasafi Festival 2018, Diamond amesema kuwa kuna wasanii wengi wakubwa huwa hawapewi nafasi ya kutumbuiza kwenye majukwaa makubwa kwa kisingizio kuwa hawajatoa nyimbo mpya.
Kaka yetu Dudu Baya muda mrefu watu hawajamuona kwenye show ya steji, sasa nawambia kwamba nitafurahi sana akiwepo kwenye show ya Wasafi Festival. Unajua sio tu Dudu Baya peke yake unajua kuna wasanii wengi wana sauti kubwa lakini sometimes hawapewi nafasi kwenye matamasha kwa sababu tu hawajatoa wimbo mwaka huu lakini kuna watu wanawapenda.“amefunguka Diamond Platnumz na kusisitiza.
so wanaoandaa Wasafi Festival nitaongea nao na Dudu Baya pia wamuweke kwenye tamasha, nitafurahi kwa sababu nilikuwa tu namuonaga kipindi kabla sijatoka namuona anaimba,“amesema Diamond

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele