Chris Brown Aweka Mambo Sawa na Mzazi Mwenzie Kuhusu Matunzo ya Mtoto

NancyTheDreamtz
Chris Brown Aweka Mambo Sawa na Mzazi Mwenzie Kuhusu Matunzo ya Mtoto
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Chris Brown pamoja na mzazi mwenza Nia Guzman kuwa wako sawa kwa sasa kwenye suala zima la utoaji matunzo kwa mtoto wao Royalty baada ya kupelekana mahakamani miezi kadhaa iliyopita.

Inaelezwa kuwa Chris Brown yupo mbioni kumnunulia Nia Guzman nyumba mpya atakayokuwa akiishi na mtoto wao Royalty mwenye umri wa miaka minne pamoja na kulipa kiasi cha zaidi ya Tsh Bilioni 2 kwaajili ya mwanasheria wa Nia Guzman.

Miezi kadhaa iliyopita Nia Guzman aliiambia Mahakama kuwa alitaka kiasi cha zaidi ya Tshs Millioni 48 kila mwezi kwaajili ya matumizi ingawa Chris Brown alikua akitoa Tsh Millioni 5 kila mwezi,

Inadaiwa kuwa wawili hao wapo katika harakati za kufuta mashtaka yanayowakabili Mahakamani baada ya miezi kadhaa kupita kuonekana kwa Chris Brown na Nia Guzman kuwa katika hali ya kuelewana kwaajili ya mtoto wao.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele