Diamond Azindua Rasmi Wasafi Festival na Wasafi FM

NancyTheDreamtz

Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB) leo imezindua kituo cha redio cha Wasafi FM pamoja na tamasha la Wasafi litakalofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa WCB, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' amesema uzinduzi wa redio hiyo unalenga kutoa fursa kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla kusikika.

"Siku ya leo redio yetu ya Wasafi FM itaanza kusikika kupitia masafa ya 88.9 katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Bado ndio tupo kwenye majaribio kwani mambo mazuri yanakuja na tumefanya hivi kwa sababu hata sisi wenyewe tulifanikiwa kwa sababu tulisapotiwa na vyombo vya habari," alisema Diamond.

Kuhusu Tamasha la Wasafi, Diamond alisema mbali ya kuburudisha, watafanya huduma za kijamii na kutangaza utalii.

"Licha kufanya tamasha, sisi tungependa kuonyesha kitu cha tofauti. Tutajitahidi katika kila mkoa tunaoenda kurudisha kwa jamii kile ambacho tunakipata kutoka kwao. Tutaangalia changamoto ya eneo husika kama itakuwa ni elimu basi tutatoa sare za shule, madawati na kadhalika. Pia tutatangaza utalii," alisema Diamond.

Kuhusu wasanii amesema wale wote wanaofanya vizuri hapa nchini watakuwepo huku akisema anatamani hata Ali Kiba naye awepo.

"Natamani kaka yangu Ali Kiba naye awepo na ninaamini uongozi wangu utaanza mazungumzo naye na huko alipo kama anafuatilia wasafi ajue tungehitaji uwepo wake, kwani inabidi tutoke kwenye muziki wa mabifu na tuingie katika kutengeneza hela na kuisaidia jamii inayotuzunguka," amesema.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele