Magufuli Ataja Fedha za Ndege Zilipotoka

NancyTheDreamtz
Magufuli ataja fedha za ndege zilipotoka
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema serikali imeweza kununua ndege kwa mara moja ni kutokana na fedha ambazo zimetokana na serikali kuwabana mafisadi.

Akizungumza wakati wa uchangiaji kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake ambapo alitaja chanzo cha fedha hizo.

“Mengine tumenunua ndege, kwa sababu watalii wetu walikuwa wachache, huwezi ukategemea shirika la ndege la jirani kuleta watalii kwenye nchi yako, tumeamua na ndio maana tumenunua ndege saba, hatukukopa nchi yoyote”, amesema Rais Magufuli

“Ni hizi hizi fedha tulizowabana mafisadi ndio tumenunua ndege, unambana fisadi anaendelea kulia kule lakini fedha unepeleka kwenye ndege wananchi wengine wananufaika, na ukilipa kwa mkupuo gharama inakuwa ndogo”, ameongeza.

Aidha Rais Magufuli kwa kipindi cha miaka mitatu serikali imefanikiwa kushughulikia masuala mbalimbali, ikiwemo utoaji wa elimu bure, na kuimarisha hali ya uchumi kwa kufufua mashirika ya umma.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais