Yanga Yafunguka Kuhusu Mchezaji wao Ibrahim Ajibu

NancyTheDreamtz
Yanga Yafunguka Kuhusu Mchezaji wao Ibrahim Ajibu
Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuwa huenda nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu amegoma kucheza kwasababu ya kutolipwa mshahara, hatimae klabu ya Yanga imethibitisha kuwa nyota wake amerejea mazoezini baada ya kupona kutokana na majeraha.


Yanga ambayo ilitoa mapumziko kwa wachezaji wake baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Lipuli FC imethibitisha kuwa leo wamchezaji wamerejea mazoezini na moja ya wachezaji walioanza mazoezi leo ni Ibrahim Ajibu na.

''Baada ya mapumziko ya siku moja kikosi kimerejea mazoezini tayari kwa mchezo wa jumapili dhidi ya Ndanda Fc. Mchezaji Ibrahim Ajibu amerejea kikosini na amefanya mazoezi na wenzake kuelekea mchezo wa Ndanda FC'', imeeleza taarifa ya Yanga.

Ajibu hajaonekana uwanjani kwenye michezo miwili ya Yanga kati ya KMC na Lipuli FC ambapo mchezo wake wa mwisho kucheza ilikuwa ni dhidi ya Alliance FC, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Baada ya mchezo huo Yanga ilitoa taarifa kuwa Ajibu alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo.

Ajibu ndiye kinara wa kutoa msaada wa mabao kwenye ligi kuu msimu huu ambapo tayari ameshasaidia mabao 7 huku yeye akifunga mabao matatu.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele