Posts

Showing posts from September, 2018

this how to Repair Printers

Image
NancyTheDreamtz

HIVI NDIVYO WEMA SEPETU ANAVYOFANYA YAKE KIMYA KIMYA

Image
NancyTheDreamtz

HOW TO WAPTRICK VIDEO

Image
NancyTheDreamtz

FOOTBALL SKILLS BY NANCY ARTHUR NYANDICHE

Image
NancyTheDreamtz

THIS IS A BONGO FLEVA HIT SONGS 2018 TANZANIA

Image
NancyTheDreamtz

Video: Wema Sepetu alivyodamshi usiku wa Birthday Gala, afunguka mengi hukumu maisha yake

Image
NancyTheDreamtz Ijumaa hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya mwanadada wa filamu, Wema Sepetu ambapo aliandaa tukio maalum Birthday Gala katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa filamu wakiwemo wasanii.

Harmonize alikaribisha kundi la muziki la Navy Kenzo WCB wasafi kwa staili ya aina yake

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na katika lebo ya muziki iliyochini ya Diamond Platnumz Harmonize ametangaza kuwakaribisha kundi la muziki la Navy Kenzo katika lebo hiyo ya Wasafi. Harmonize alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuwa karibuni ” Nisaidieni kuwakaribisha NavyKenzo usafini mimi huwa sipendagi mambo ya siri siri kwani tunamuogopa nani ???? Welcome to the family #WCB4LIFE” lakini baada ya kutangaza kuwakaribisha wasanii hao wawili nao wali-reply kwa Harmonize Aika akiandika huku akianza na kuweka emoji za kucheka ” Ni usafi tu ” na kumtag tena Harmonize. Kundi hilo la Navy Kenzo linaundwa na wasanii wawili ambao ni Nahreel pamoja na mke wake Aika,lakini pia likiwa chini ya meneja Sallam Sk ambaye pia ni meneja wa C.E.O wa lebo ya Wasafi namaanisha Diamond Platnumz. Kupitia ujumbe huo wa Harmonize inawezekana tukaanza kuwaona Navykenzo yaani Aika na Narel wakianza kufanya kazi na kutoa nyimbo wakiwa chini ya WCB Wasafi...

MUSIC VIDEO: Mycoely – Ringa

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mycoely anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya wa Ringa, Kichupa kimeongozwa na Adam Juma. Enjoy!

Kwa hiki alichoposti msemaji wa Yanga ni ishara ya matokeo ya kesho dhidi ya mnyama Simba ?

Image
NancyTheDreamtz Kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby hapo kesho ambao utawakutanisha miamba ya soka nchini Simba SC dhidi ya Yanga, msemaji wa wanajangwani Young Africans, Dismas Ten ameandika ujumbe kwenye ukurusa wake wa kijamii wa Instagram unaoashiria matokeo yatakavyokuwa baada ya mechi hiyo. Ten ameandika ujumbe mfupi kwenye ukurasa huo wa Intsagram unaosomeka 1 – 4 ambayo namba moja inawakilisha rangi nyekundu ya watani zao Simba huku namba nne ikiwakilisha rangi ya Yanga. Kumekuwa na utani wa hapa na pale kila inapokaribia mechi ya watani hawa wa jadi aidha iwe kwenye ligi kuu ama mashindano mengine na matokeo ya mchezo wao huwa hayaamuliwi kwa ubora wa timu fulani au ukubwa wa usajili wake na kharama zilizotumika bali siku zote huwa ni matokeo ya kushangaza. Simba itakuwa mwenyeji kwenye mchezo huo wa hapo kesho ambao unatarajiwa kuchezwa majira saa 11 za jioni huku mgeni ramsi akiwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

Tazama Hapa Video ya Navy Kenzo ft. Diamond Platnumz - Katika

Image
NancyTheDreamtz Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo wameachia video ya wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la  Katika  ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz. Itazame hapa. By Nancy Arthur Nyandiche

Papa Francis awatambua na kuwaridhia maaskofu saba walioteuliwa China

Image
NancyTheDreamtz Makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican na China zimetangaza juu ya kutiwa saini mkataba wa kihistoria, wa muda mfupi uliofikiwa kati ya pande hizo mbili kuhusu uteuzi wa maaskofu nchini China. Papa Francis amekubali uhalali wa maaskofu saba wa China, walioteuliwa na China bila idhini ya Vatican. Hatua hiyo imemaliza mzozo wa kidiplomasia uliokuwepo kwa miongo kadhaa na ambao umesababisha mgawanyiko miongoni mwa waumini wa Kikatoliki nchini China. Ni miongo saba sasa tokea Vatican na China zikate mahuasiano rasmi kati yao. Uamuzi huo ni sehemu ya makubaliano ya kihistoria kati ya Kanisa Katoliki na China juu ya uteuzi wa maaskofu, jukumu ambalo kwa kawaida huwa la Papa. Mkataba huo wa muda ulisainiwa mjini Beijing na kutangazwa wakati Papa Francis alipokuwa anafanya ziara nchini Lithuania ikiwa ni mwanzoni mwa safari yake ya siku nne katika mataifa yanayoizunguka bahari ya Baltic, kaskazini mwa Bara la Ulaya. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican, Papa Franc...

Sitaki kuolewa tena na kijana, nataka mwanaume mzungu aliyeachika – Hamisa Mobetto

Image
NancyTheDreamtz Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka wazi mwanaume ambaye anataka kuishi naye kwa sasa, ambapo amedai kuwa anataka mwanaume wa kizungu ambaye alishawahi kuachika na mwenye watoto. Hamisa Mobetto Akizungumzia vigezo vya mwanaume anayemtaka, Hamisa amesema kuwa kwa sasa hapendi kuolewa na vijana na anatafuta Mzungu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 45. “ Mimi hapa nataka labda mzungu au mtu mzima,  awe alishawaki kuachwa au Mgane kwa hiyo ndio hivyo, yaani nikisema kijana dah hapana. Awe angalau miaka 45 kwa sababu mimi mwenyewe nina watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wangu, “amesema Hamisa Mobetto kupitia EATV. Hamisa Mobetto tayari ameshazaa watoto wawili na wanaume wawili tofauti tofauti, ambao ni Diamond Platnumz na Majizzo na amesema kwa sasa hawezi kurudiana na yeyote kati yao. Kwa upande mwingine, Hamisa Mobetto amekiri kuwa sauti iliyosambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita akiongea na Mganga wa kienyeji...

Wamiliki wa Blog ya Dauda.com waachiwa kwa dhamana Mahakama ya Kisutu

Image
NancyTheDreamtz Wamilikiwa wa blog ya Dauda.com  wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mkazi Kisutu ambao ni pamoja na mtangazaji wa Clouds fm Shaffih Dauda. Wawili hao wanatuhimiwa kwa kosa la kuendesha blogs bila kuwa na kibali. Licha ya Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 mwezi wa kumi,washtakiwa hao walikataa tuhuma hizo za kumiliki blog bila kuwa na kibali. Wakili wa upande wa Jamhuri ameiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kwa Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambone ameiomba Mahakama kuwapa dhamana wateja wake kwa kuwa haki ya kupata dhamana ipo na Hakimu wa kesi hiyo amekubali kuwapa dhamana washtakiwa hao. Shafiih na wenzake ambaye anashikiliwa ni Ben Ali (Ben On Air) ambaye alikuwa muendeshaji wa Dauda TV kupitia mtandao wa (Youtube) walikamatwa wiki iliyopita kwa kosa la kuendesha blog hiyo bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Afya ya Haji Manara yatetereka, mwenyewe adai amelishwa sumu na sio presha ya matokeo ya Simba

Image
NancyTheDreamtz Baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameshikwa na presha iliyopelekea kulazwa mkoani Shinyanga, hatimaye mwenyewe aweka wazi kinachomsumbua. Haji Manara Manara amesema kuwa alikula chakula chenye sumu, na ndio sababu iliyompelekea kulazwa na sio presha ya matokeo mabaya ya klabu yake kama inavyoandikwa mitandaoni. “ Siumwi pressure wala moyo kama inavyoandikwa mitandaoni..nahic nimepata food poisoning na niwashukuru Madaktari walionihudumia awali Shinyanga na Mwanza ..now nisharejea Dar teyari kwa vipimo zaidi…Insha’Allah kila kitu kitazidi kuwa salama, “ameeleza Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram. Klabu ya Simba imekuwa na matokeo mabovu kwa msimu huu ambapo wiki iliyopita imepokea kichapo cha goli 1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Wanaharakati hawa watatu watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel wakiwa Jela

Image
NancyTheDreamtz Wanaharakati watatu wa haki za binadamu kutoka Saudia walioko jela watunukiwa tuzo mbadala ya Nobel na taasisi ya Nobel mjini Stolkholm.Pia wapinga rushwa kutoka Guatemala watunukiwa tuzo ya heshima. Washindi wa tuzo maalum ya haki za binadamu au tuzo mbadala ya Nobel wametangazwa leo hii mjini Stolkholm Sweden. Tuzo hiyo imetunukiwa watetezi watatu wa haki za binadamu wakisaudi waliofungwa jela pamoja na wanaharakati wa kupinga rushwa kutoka Amerika Kusini. Taasisi ya tuzo hiyo mjini Stolkholm imesema dolla 113,400 zinazoambatana na tuzo hiyo mbadala ya Nobel zitagawanywa kwa washindi Abdullah al Hamid,Mohammad al-Qahtani na Waleed Abu al Khair wote wa Saudi Arabia kutokana na juhudi zao za kijasiri zinazosimamia misingi ya haki za binadamu ya kimataifa,ili kuleta mageuzi katika mfumo wa kidhalimu wa kisiasa nchini Saudi Arabia. Tuzo  ya heshima ya mwaka huu imetunukiwa Thelma Aldana wa Guatemala na mkolombia Ivan Velasquez kutokana na mchango wa...

Maua Sama na Soudy Brown kuendelea kusota mahabusu (Audio)

Image
NancyTheDreamtz Mwanamuziki Maua Sama Jumatatu hii hajapandishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa na wadau wengi huku wenzake Soudy Brown akipandishwa mahakamini na kusomewa shtaka moja la kutumia mitandao ya kijamii bila kuwa na kibali. Wawili hao kwa pamoja walikamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita kwa tuhuma za kuidhalilisha nembo ya Taifa baada ya kupost video moja mtandaoni inayowaonyesha watu wakichezea hela za Tanzania. SoudyBrown amesomewa shtaka moja la kuweka maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali lakini dhamana ya kosa hilo iko wazi lakini anadaiwa bado anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu. Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo Augustine Rwizile ameghailisha kesi hiyo hadi 18 October 2018. Naye Maua Sama hakuletwa mahakamani leo kama watu walivyotarajia huku wadau wa mambo wakidai kesi yake nitaanza kusikilizwa katikati ya wiki hii. Mmmoja kati ya mawakili ambao walijitokeza mahakamani hapo walidai wamewasiliana na jeshi la p...

Hamisa Mobetto atua Kenya na kupokewa mchekeshaji huyu (Audio)

Image
NancyTheDreamtz Mwanadada Hamisa Mobetto Jumatatu hii ametua nchini Kenya na kupokelewa na mchekeshaji, ChipuKeezy ambaye kwa sasa anaendesha kipindi kimoja cha TV nchini humo. Hatua hiyo ni siku moja toka Diamond ampost mama watoto wake wa zamani Zari na kueleza kwanini hawezi kuanika mambo ya Zari mtandaoni tofauti alivyofanya kwa Mobetto. Wawili hao waliingia kwenye mgogoro wa kutupiana maneno toka Diamond anyake sauti ya Mobetto akizungumza na mtu anayedaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji. Rel

Huyu ndio mrithi mpya wa Zari na Hamisa Mobetto kwa Diamond Platnumz ? (Audio)

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa muziki wa kizazi kipya na C.E.O wa lebo ya muziki ya Wasafi Diamond Platnumz amekuwa ni mtu wa matukio kila siku kukicha. Msanii huyo asiyeishiwa matukio kwenye mitandao ya jamii bado anaendelea kuwa gumzo mitandaoni baada ya kupost video inayomuonyesha mwanadada mmoja ambaye jina lake halijajulikana mpaka hivi sasa na kuandika caption yeye utata akiweka imoji zenye kuonyesha upendo huku akiweka hashtag “Usingiz” huku wasanii na wadau mbalimbali wa sanaa wakicoment chini ya video hiyo wengine wakiandika Simba mla nyama. Tukio hilo halikuishia hapo kwa mama yake Diamond mama Dangote aliirepost video hiyo na maneno yale yale ya Diamond ila yeye akaweka hashtag yake na kuandika “Mmemaliza kuchamba”

Bobi Wine afanya kufuru kwa vijana katika jimbo lake jijini Kampala

Image
NancyTheDreamtz Mwanamuziki na mbunge nchini Uganda, Bobi Wine amemkejeli rais Yoweri Museveni, kwa kutoa mchango wa dola 26,000 ambazo ni sawa na milioni 59 za kitanzania kwa vijana katika eneo bunge lake mjini Kampala. Kwa mujibu wa ripoti katika televisheni ya NTV Uganda, Bobi Wine amesema ”Kwa kuwa serikali haina la kuwaambia watu, sasa imegeukia kuwanunua-wakiona hamtishwi na risasi wanawarushia pesa” Bobi pia amesema kuwa ”Utawala hauamini kuwa mtu anaweza kuzungumza na watu bila kuwarushia pesa” Mwanasiasa huyo anadai kuwa serikali ilijaribu kuipatia pesa familia ya dereva wake aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agost 13.Gazeti la Daily Monitor pia limeangazia madai hayo likisema familia ya dereva huyo aliyeuawa ilikataa kupokea pesa hizo. Bobi Wine pia alidai kuwa ni yeye aliyekuwa analengwa katika kisa cha kupigwa risasi na kuuawa kwa dereva wake Bobi Wine, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na kupigwa mawe msafara ...

Audio: Diamond sio husband material, ametembea na wengi sana – Hamisa Mobetto

Image
NancyTheDreamtz Mwanamitindo Hamisa Mobetto amedai mzazi wenzake Diamond Platnumz sio aina ya wanaume ambaye alikuwa anamwitaji katika maisha yake. Amedai muimbaji huyo ni mwanaume wa kutembea na wanawake wengi na hawezi tulia na mmoja huku akidai nchini Tanzania ametembea na wanaume wengi sana. Related Articles

Kwa jeuri hii ya fedha aliyoionesha Davido, angekuwa Bongo angepata tabu sana (+Audio)

Image
NancyTheDreamtz Msanii kutoka Nigeria, Davido jana ameonesha jeuri ya fedha kwa mara nyingine baada ya kuwanunulia members 18 wa 30 Billion Gang toleo jipya la simu za iPhone XS. Davido kupitia Insta Story alionesha simu hizo na kusema kuwa amenunua kwa ajili ya watu wake wote wa 30 Billion Gang akiwemo mchumba wake, Chioma . Toleo hilo la iPhone XS ndio toleo jipya la simu hizo pendwa duniani, na simu moja inauzwa dola $1,400 ambayo ni sawa na Tsh milioni 3. Kwa hesabu ndogo Davido ametumia tsh milioni 54 kuwanunulia simu rafiki zake ambao wanaunda kundi hilo la 30 Billion Gang. 30 Bilion Gang ni kundi ambalo Davido ndio kiongozi lakini pia wapo binamu zake wawili Sina Rambo na B-Red na meneja wake Asa Asika. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake wameshusha maombi wakitaka nao wapewe zawadi za simu hiyo mpya  ya iPhone XS. mrbrownchips @davidoofficial  boss abeg bless me with phone…I saw the ones you got for your team…me na your team too abeg. youngwiz_of...

Meli iliyopata ajali miaka 400 yapatikana, inadaiwa ilikuwa njiani kutoka India

Image
NancyTheDreamtz Watafiti wa mambo ya kale wamegundua meli iliyopata ajali miaka 400 iliyopita karibu na pwani ya Ureno, katika tukio ambalo wataalam wameliita “ugunduzi muhimu”. Kwa mujibu wa mtandao wa REUTERS, baadhi ya viungo, vyombo vya kauri na mizinga ikiwa na nembo ya Ureno vimetapakaa katika eneo la karibu na Cascais ambapo si mbali sana kutoka Mji Mkuu Lisbon. Wagunduzi hao waamini kwamba meli ilikuwa njiani kutoka India wakati ilipozama kati ya mwaka 1575 na 1625. Nyakati hizo zinakadiriwa kuwa ndiyo kilele cha biashara ya viungo kati ya Ureno na nchi za Asia. Inadhaniwa kuwa huu ni ugunduzi mkubwa kabisa ambao umechukua takribani miaka 10 kwa mujibu wa mkurugenzi wa zoezi hilo, Jorge Freire ambapo akisisitiza ni jambo muhimu zaidi kwa Ureno.

Simba Yaenda Kuweka Kambi Zanzibar Kwaajili ya Kupambana na Yanga

Image
NancyTheDreamtz Kikosi cha Simba kinaondoka leo jijini Dar es Salaam kuandaa dawa maalum ya kuwamaliza Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Septemba 30 Jumapili hii. Simba wanaenda kuweka kambi hiyo Zanzibar kama ilivyo mara nyingi pindi wanapojiandaa kucheza na Yanga tayari kuja kukabiliana na watani zao wa jadi walio na alama 12 kileleni. Kuelekea mchezo huo, wachezaji wa kikosi cha timu hiyo waliokuwa Dar es Salaam kwa ajili ya program maalum iliyokuwa chini  ya Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, wataungana na wenzao visiwani humo. Wachezaji hao ambao miongoni mwao ni Haruna Niyonzima na Juuko Murushid wataongeza nguvu kwa ajili ya kujifua vilivyo kuelekea mechi hiyo. Ikumbukwe Simba inaenda kucheza na Yanga ikiwa na kumbukukumbu ya ushindi katika mchezo wao wa mwisho kwa bao 1-0 msimu uliopita.

Wasanii Wengi Hawaweki Maisha yao Halisi Katika Mitandao:-JB

Image
NancyTheDreamtz Msanii wa bongo movies jacob steven amefunguk na kusema kuwa wasanii wengi wa bongo movies wako tofauti sana  na wale wa bongo fleva kwa sababu hawaweki uhaisia wa maisha yao na kazi yao katika mitandao yya kijamii kitu ambacho kiko tofauti sana. JB anasema kuwa ukiangaia profile nyingi za bongo fleva artst utagundua tu kwa urahisi kuwa huyu ni msanii wa muziki lakini inakuwa ngumu sana kwa wale waigizaji kuweka profile yake hadharani kama wanavyofanya wengine. akiongea na waandishi wa habari JB Anasema ‘wasanii wengi wa bongo movies hawawekagi maisha yao halis katika mitandao, tofauti sana na wale wa bongo fleva ambao wao  ukichungulia tu akaunti zao unakuwa unajua kuwa huyu ni msanii.hii yote ni kwa sababu ya watazania wengi ni malimbukeni wa matumizi ya mitandao ya kijamii.’ Ujumbe huu wa JB unawaendea moja kwa moja wasanii wanaotaka kuishi maisha  ambayo sio ya kwao, Jb anasema kuwa ni bora kuwa muwazi ili shabiki anapoamua kukukubali basi inakuwa ...

Zoezi la Kubinua Kivuko cha MV. NYERERE Limefikia Pazuri..Tazama Video

Image
NancyTheDreamtz Leo September 24, 2018 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Venance Mabeyo amesema zoezi la kukinasua Kivuko cha Mv. Nyerere limefikia pazuri tayari wamekiinua upande mmoja na wana matumaini kitatoka vizuri. “Wameanza kukinyanyua kwenye injini, ili kukinyanyuliwa kije juu kielee lakini sasa kinafungwa maboya kwa chini, tunaandaa pampu ili kikichota maji yaweze kunyonywa, tuwe na matumaini kivuko kitatoka vizuri” -Mabeyo VIDEO: