Harmonize alikaribisha kundi la muziki la Navy Kenzo WCB wasafi kwa staili ya aina yake

NancyTheDreamtz
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na katika lebo ya muziki iliyochini ya Diamond Platnumz Harmonize ametangaza kuwakaribisha kundi la muziki la Navy Kenzo katika lebo hiyo ya Wasafi.
Harmonize alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuwa karibuni ” Nisaidieni kuwakaribisha NavyKenzo usafini mimi huwa sipendagi mambo ya siri siri kwani tunamuogopa nani ???? Welcome to the family #WCB4LIFE”
lakini baada ya kutangaza kuwakaribisha wasanii hao wawili nao wali-reply kwa Harmonize Aika akiandika huku akianza na kuweka emoji za kucheka ” Ni usafi tu ” na kumtag tena Harmonize.
Kundi hilo la Navy Kenzo linaundwa na wasanii wawili ambao ni Nahreel pamoja na mke wake Aika,lakini pia likiwa chini ya meneja Sallam Sk ambaye pia ni meneja wa C.E.O wa lebo ya Wasafi namaanisha Diamond Platnumz.
Kupitia ujumbe huo wa Harmonize inawezekana tukaanza kuwaona Navykenzo yaani Aika na Narel wakianza kufanya kazi na kutoa nyimbo wakiwa chini ya WCB Wasafi.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele