Kwa hiki alichoposti msemaji wa Yanga ni ishara ya matokeo ya kesho dhidi ya mnyama Simba ?

NancyTheDreamtz
Kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby hapo kesho ambao utawakutanisha miamba ya soka nchini Simba SC dhidi ya Yanga, msemaji wa wanajangwani Young Africans, Dismas Ten ameandika ujumbe kwenye ukurusa wake wa kijamii wa Instagram unaoashiria matokeo yatakavyokuwa baada ya mechi hiyo.
Ten ameandika ujumbe mfupi kwenye ukurasa huo wa Intsagram unaosomeka 1 – 4 ambayo namba moja inawakilisha rangi nyekundu ya watani zao Simba huku namba nne ikiwakilisha rangi ya Yanga.
Kumekuwa na utani wa hapa na pale kila inapokaribia mechi ya watani hawa wa jadi aidha iwe kwenye ligi kuu ama mashindano mengine na matokeo ya mchezo wao huwa hayaamuliwi kwa ubora wa timu fulani au ukubwa wa usajili wake na kharama zilizotumika bali siku zote huwa ni matokeo ya kushangaza.
Simba itakuwa mwenyeji kwenye mchezo huo wa hapo kesho ambao unatarajiwa kuchezwa majira saa 11 za jioni huku mgeni ramsi akiwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele