Wema Awapa Pole Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mume Wake Mtarajiwa

NancyTheDreamtz

Mwanadada Wema Sepetu ambae wiki iliyopita aliacha gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumuweka wazi mwaaume ambae alijulikana kwa jina la Patrick christopher na kusema kuwa huyo ndio mume wake mtarajiwa.

Baada ya kuweka picha hizo wakwa faragha na mume wake huyo , watu walianza kuongea maneno mengi katika mitandao huku baadhi ya mahasimu wake wakijitahidi kutafuta mabaya ya wema na hata ya mwanaume huyo na kuyaweka hadharani.
Hata hivyo Wema haonekani kujali maneno yoyoote anayosema kuhusu mwanaume huyo na amesema kuwa hata kama wataungana dunia nzima kwake ni kazi bure tu hivyo waache kuongea maana hakuna kinachosaidia .

Akiongea na waandishi wa habari Wema anasema “yaani watu wametokwa na povu kama lote kisa mimi kumunyesha mume wangu tu, sasa hata wakiungana dunia nzima kunisema kama nimeshampenda watanibadilisha vipi”

Mwanaume huyo amekuwa akikoselewa sana na hata kuonyeshwa baadhi ya vitu kama kuwa na familia na watoto alipwatelekeza, lakini pia inasemekana kuwa mwanaume huyo ambae ni raia wa Burundi amekuwa akitafutwa huko kwao kwa kosa la utapeli.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele