BASATA Wakanusha Kumuita na Kumhoji Wema Sepetu

NancyTheDreamtz
BASATA wakanusha kumuita na kumhoji Wema Sepetu
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limekanusha taarifa ambazo zinazagaa mtandaoni kwamba wamemuita malkia wa filamu Tanzania, Wema Sepetu kutokana na kusambaza video mtandaoni akila denda na mwanaume aliyedai ni mpenzi wake mpya.

Wiki iliyopita muigizaji huyo aliachia video hiyo na picha za mwananume huyo akidai ameshindwa kulizuia penzi lake hilo kwa mwanaume huyo.

Baada ya kugaa kwa taarifa hizo, chombo kimoja cha habari kilizungumza na Afisa Habari Basata, Agness na kukanusha taarifa hizo huku akidai kama mwanadada huyo anaenda Basata ni kwa mambo yake binafsi sio kwamba aliitwa.

“Sio kweli Wema ameitwa Basata, hata sisi tunasikia hizo habari na kuihusisha na mambo yake ya kwenye mitandao, sisi kama Basata atu-deal na maisha binafsi ya wasanii labda afanye tukio katika kazi ya sanaa ndio tunaweza kumuita,” alisema Agnes “Kama ni mambo ya mtandaoni TCRA ndio wenye mamlaka,”

“Basata ni sehemu ya wasanii, ni wazazi wa wasanii, kama anakuja sisi tutampokea na kuzungumza naye hukusu sanaa yake na namna ya kujiweka kama msanii lakini mpaka sasa hatuna taarifa kama anakuja lakini akija sawa tutampokea,”

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele