Ronaldo Aingia na Saa ya Mabilioni Old Trafford

NancyTheDreamtz
Ronaldo aingia na saa ya mabilioni Old Trafford
Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo ameingia na saa ya dhahabu katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya wenyeji Manchester United.


Saa aliyoivaa Cristiano Ronaldo kwenye mkutano na wanahabari

Saa hiyo inaelezwa kuwa imebuniwa na mbunifu, Francky Muller na kutengenezwa na kampuni ya Jacob&Co Carviar Tourbillon Range.

Kwa mujibu wa ripoti, aina hiyo ya saa pia iliwahi kuvaliwa na msanii maarufu wa muziki wa Nigeria, Wizkid ambapo inadaiwa aliinunua kwa dola 1.2 milioni ambazo ni sawa na Sh 2.7 bilioni za kitanzania.

Hilo ni toleo jipya la saa za kampuni hiyo, ambapo awali iliwahi kumtengenezea nyota huyo saa yenye thamani ya pauni 100,000 ambazo ni sawa na sh 297 milioni za kitanzania.

Manchester United na Real Mdrid zinatarajia kukutana usiku wa leo katika mchezo wa hatua ya makundi ya klabu bingwa Ulaya huku Cristiano Ronaldo akirejea katika uwanja wa Old Trafford akiwa na klabu ya pili tofauti tangu alipoondoka mwaka 2009.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele