Lema Afunguka Mazito Baada ya Kuhojiwa na Polisi "Bado Nautafakari Muujiza wa Mo Dewji Kutekwa Colosseum na Kurudishwa Gymkhana"

NancyTheDreamtz
Lema Baada ya Kuhojiwa na Polisi Afunguka Haya "Bado Nautafakari Muujiza wa Mo Dewji Kutekwa Colosseum na Kurudishwa Gymkhana"
Mbunge wa Arusha Mjini na waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Mh Godbless Lema amefunguka baada ya kuhojiwa na polisi na kusema kuwa amehojiwa kuhusiana na  tukio la kutekwa na kupotea  kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Lema amesema kuwa aliitwa kuisaidia polisi na kutoa maelezo kama aliyoyatoa siku alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya sakata hilo.

"Nilitoa maelezo kama yale ambayo niliongea kwa waandishi wa habari ila nimelishauri kuwaacha huru watu kutoa maoni kwani mzalendo wa kweli ni yule ambaye anayeongea wakati mambo hayaendi sawa lakini si yule anayenyamaza mimi ni mzalendo wa kweli na nitaendelea kukosoa kama waziri wa mbambo ya ndani lakini kama Raia mzalendo wa hichi pale mambo kama haya yataendelea.

Aliendelea kusema kuwa kwa namana alivyotekwa Mo na kurudishwa ni kitu cha kihistoria.

"Mo Dewji alitekwa karibu na makamu ya Rais na alipatikana karibu na ikulu huu ni muujiza mkubwa na nitazidi kuutakafari muujiza huu na kama tajiri unatekwa Collessium Hotel na Unarudishwa Gymcanas Hotel huu ni muujiza mkubwa na nitaendelea kuutafakari"

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lema ameandika; Polisi wameniuliza maswali juu ya utekwaji wa Mo. Nimesema kuwa kutekwa kwa Mo na kupatikana kwake kumeacha wasiwasi mwingi. Naamini kama biblia ingekuwa bado inaandikwa pengine suala hili lingeandikwa kama muujiza,” amesema Lema.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele