Mume wa Bi Sandra Akwaa Skendo Nzito

NancyTheDreamtz
Mume wa Bi Sandra Akwaa Skendo Nzito
MUME wa Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye ni mama wa mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Maisala Shante ‘Anko’ amekwaa skendo ambayo huenda ikatikisa ndoa yake. 



Skendo hiyo inamganda kufuatia gazeti hili kunasa sms tata alizokuwa akizituma kwa mama mmoja mke wa mtu, (jina tunalihifadhi kwa sasa) huku ikishindwa kufahamika ukaribu wao huo unakujaje wakati wote wana watu wao.

KUVUJA KWA SMS HIZO

Awali chanzo chetu cha kuaminika kilitutonya kuwa, kina meseji zinazomuonesha Anko akichati na mwanamke ambaye ni mke wa mtu ila kikaomba hifadhi ya jina lake kuepuka shari. “Usije ukaniuliza nimezipatapataje na sitaki mnitaje ila nina meseji za yule mume wa mama Diamond akimtumia mke wa mtu,” alidai sosi huyo.

Risasi: Wewe umezipatapataje kwani?

Sosi: Kuna shosti wangu anajuana na huyo mke wa mtu, sasa sijui kazichukua vipi kwenye simu yake. Mimi nimeona ni stori, au unasemaje?

Risasi: Ni stori ndiyo, meseji zenyewe zikoje?

Sosi: Wewe niambie mtanilipaje nizilete, uzione tuongee biashara.

Risasi: Njoo basi ofisini, sisi tuko Sinza Mori hapa.

Baada ya nusu saa

Kuonesha kuwa, mtoa habari huyo hakuwa mbali na ofisi zetu, ndani ya nusu saa alikuwa ameshafika na kumuonesha mwandishi wetu SMS hizo ambazo zilionesha dhahiri kutoka kwa Anko kwenda kwa mke wa mtu huyo.

MESEJI ZIKOJE?

Ukifuatilia ‘chating’ za wawili hao utabaini wana ukaribu wa kupitiliza kwani, mbali na sms za kawaida, kuna wakati mwanaume huyo alikuwa akimtumia video za kimahaba na picha sambamba na maneno matamu. Gazeti hili haliwezi kuchapisha meseji hizo kutokana na sababu za kisheria ila ifahamike tu kwamba, chating hizo tunazo.

MKE WA MTU ASAKWA

Baada ya kuzinasa sms hizo na kuthibitisha kuwa ni kweli zilikuwa ni za Shamte na mke wa mtu huyo, paparazi wetu alifanya jitihada za kuwapata wote wazungumzie kilichopo kati yao. Wa kwanza kutafutwa alikuwa mwanamke ambaye alipopokea mahojiano yalikuwa hivi:

Risasi: Haloo, habari yako dada

Mke wa mtu: Njema, naongea na nani?

Risasi: Mimi naitwa… (mwandishi anataja jina lake) ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Risasi.

Mke wa mtu: Unasemaje?

Risasi: Sasa dada, tumenasa mawasiliano yako na mume wa mama Diamond na inaonekana mna ukaribu uliopitiliza, kwani mkojemkoje?

Mke wa mtu: Mmenasa meseji zangu nikichati na nani?

Risasi: Na yule mume wa mama Diamond, Shamte.

Mke wa mtu: Sikia wewe, kwanza nitahakikisha nakupata maana simu yangu iliibwa kwa hiyo wewe utakuwa unamjua mwizi.

Risasi: Sawa dada ila ni kweli una uhusiano na Shamte?

Mke: Nimekuambia simu yangu ilipotea, unachoniambia mimi sikikumbuki kabisa kama niliwahi kuchati na huyo mwanaume chochote, lakini pia kama nitakuwa nimechati naye kuna ubaya gani, si mwanaume kama wanaume wengine.

SHAMTE HUYU HAPA

Baada ya mwanamke huyo kubanwa na kufunguka hayo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Shamte ambaye alidai kuwa hana tabia za kuchati na wanawake. “Nakuheshimu kama mwandishi kukujibu swali hili, mimi sijawahi kuchati na wanawake ovyo, kama una namba ya huyo mwanamke nitumie ndio nitakujibu,” alisema Shamte.

TUJIKUMBUSHE

Shamte ni mume halali wa Mama Diamond, walifunga ndoa mwaka jana na baada ya ndoa hiyo kukazuka ‘vijineno’ ikiwemo madai kuwa mwanaume huyo ni marioo na ndoa yao haitadumu. Hata hivyo, wawili hao wameendelea kuwa pamoja na kuwafanya watu waamini kwamba, kweli mapenzi hayachagui umri, kikubwa ni kuwepo kwa mapenzi ya kweli.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele