Jose Morinho Amtafuta Mchawi wake ndani ya United, Adai Haiwezekani Siri yake Kuvuja Mitandaoni

NancyTheDreamtz
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameanzisha uchunguzi ndani ya timu hiyo kufahamu aliyetoboa siri ya orodha ya kikosi chake ‘line-up’ alichokipanga kwaajili ya kuikabili Chelsea mchezo uliyomalizika kwa sare ya mabao 2 – 2 Jumamosi iliyopita.

Mourinho alitoka kwenye hoteli waliyofikia na kwenda kutafuta ukweli juu ya aliyetoboa siri hiyo na kuposti kwenye mitandao ya kijamii kikosi chake cha wachezaji 11 alichokipanga.

Mourinho na kikosi chake walipigwa picha wakati wakitoka kwenye kituo cha treni cha Stockport siku ya Ijumaa walipokuwa wakielekea kwenye hoteli ya Pestana kwaajili ya kuikabili Chelsea.

Hata hivyo inaelezwa kuwa wachezaji na baadhi ya wafanyakazi pekee ndiyo waliyojua kikosi kitakachoanza siku hiyo dhidi ya Chelsea kabla ya kusambaa kwake kwenye mitandao.

Hii ni mara ya pili kwa kikosi cha Manchester kuvuja kabla ya mechi iliwahi kutokea hata walipokwenda kuikabili West Ham mwezi uliyopita.

United iliyokuwa na mwanzo mbaya katika dakika 45 za kipindi cha kwanza Stamford Bridge kabla ya kujipanga kipindi cha pili, wachezaji walirejea Manchester siku ya Jumamosi huku wakionekana kukata tamaa baada ya kulazimishwa sare kwenye dakika za ziada kabla ya mchezo huo kumalizika.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele