Ruge Mutahaba na Nikki wa Pili watoa neno kwa muandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2018
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
-
NancyTheDreamtz
Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nikki wa Pili wamemmwagia sifa za kutosha Muandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2018, Basilla Mwanukuzi.
Basilla Mwanukuzi.
Ruge kwenye barua yake ya pongezi amesema Bi. Basilla amerudisha heshima ya shindano hilo ambalo lilikuwa linaonekana kupoteza sifa yake kwa miaka ya hivi karibuni.
“Basila Hongera sana mdogo wangu, kikubwa ulichofanikisha kufanya ni kuanza kurudisha imani kwa waliopoteza imani na hiyo brand. Sio siri, itakuchukua mwaka mmoja, miwili hata mitatu kufika kwenye level ya kupata the same integrity na value iliyokuwa imepotea. Kurudisha imani za wadhamini, wahisani na mwisho sisi wananchi tutarudi labda kwa ukubwa kuliko ilivyokuwa. Umefanya makosa mengi sana kwenye hii hatua ila ni sehemu ya ukuaji because najua hakuna mtoto anajaribu kutembea bila kuangukaanguka. Kama Clouds Media Group tupo na wewe na mawakala wote kwa pamoja mmewezesha jambo hili kurudi kupata heshima yake. Kubwa kuliko yote ili kujenga heshima inayodumu ungalizi wa washindi uendelee kwa muda mrefu kupata role models wengi kwa taifa letu. Mungu awabariki sana.“ameeleza Ruge.
Kwa upande mwingine, Nikki wa Pili naye amemmwagia sifa muandaaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “nimpongeze mwandaaji wa miss tanzania @basillamwanukuzi kwanza kwakuwa ni mwanamke(yes) pili kuona fursa katika passion yake ya urembo, tatu kuirudisha misstanzania iliyo kuwa imepotea, nne kwa kuanza na kidogo lengo si zawadi lengo kujenga brand ya misstanzania na warembo pia……..Nachosema songa mbele ifanye kuwa taasisi itengeneza pesa na ajira mwaka mzima…….warembo wa 5 waliopata ajira nao wata tengeneza ajira kwa wapiga picha, wabunifu, na watu wa branding, media zimepata content, biashara zimetangazwa, watu wamepata burudani na fursa kibao umezifungua ni kwa vijana kufikiria kuziendeleza kutokea jana kwenda mbele..#wenye wingi wa lawama wana uchache wa kuona fursa.“.
Jana usiku kulikuwa na shindano la Miss Tanzania 2018 ambapo mrembo, Queen Elizabeth aliibuka kidedea kwa kuwamwaga wenzake 19.
NancyTheDreamtz Huu kwa mujibu wa utafiti wa kabila zilizotoa wasomi wengi nchini tanzania. 1.wahaya wanapatikana mkoani kagera wakitokea bukoba na sehemu zingine za mkoa huoo 2.wagitaa wanapatikana wilaya ukerewe na musoma mjini na vijini mkoani mara 3.wachaga mkoani kilimanjaro wa wilaya ya moshi mjini,marangu,hai na sehemu zingine 4.wanyakyusaa mkoani mbeya wapo haswa wilaya ya kyela,songwe na zinginezo. 5.wakurya mkoani mara wilaya ya tarime na serengeti 6.wajaluo mkoani mara wilaya ya rorya na serengeti pia 7.wangoni wanatokea mkoa wa ruvuma 8.wapare wanatokea mkoa kilimanjaro wilaya ya same. 9.wasukuma hawa wapo mwanza na shinyanga 10.wanyamwezi hawa wanatokea mkoani tabora
NancyTheDreamtz Mshambuliaji hatari ndani ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa kabla ya maisha yake ya soka alitamani kuwa mwanajeshi. Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiwaacha washabiki wake na swali. Muda mwingine mungu akupi unaloliomba ila anakupa linalo kustahili… Kabla ya soka,nilikuwa natamani kuwa mwanajeshi,je kwa sura hii unadhan ningependeza kuwa soja? Kwa sasa nyota huyo yupo njiani akielekea nchini Uganda akiwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars kwaajili ya kuikabili timu ya Uganda ‘The Cranes’ ikiwa ni mchezo wa kuwania kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon utakao pigwa siku ya Jumamosi ya Septemba 8 mwaka huu 2018.
MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva, Benham Paul ‘Ben Pol’, usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2021 amefanya shoo ya aina yake jijini Mwanza kwenye tamasha lake la Nandy Festival 2021. Nandy, amesindikizwa na wanamuziki wengine akiwemo Baba Levo, Fid Q, Meja Kunta na wengine. NancyTheDreamtz
Comments