Muigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael amaliza kimya chake cha mwaka mmoja mitandaoni, amuandikia ujumbe mzito Majizzo
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
-
NancyTheDreamtz
Baada ya kimya cha muda mrefu cha takribani siku 324 mitandaoni, hatimaye Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael almaarufu Lulu amerudi rasmi kwa kumuandikia ujumbe mahsusi mpenzi wake Majizzo ambaye pia ni Mkurugenzi wa EFM na TV-E .
Majizzo na Lulu
Lulu ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika, “Lover,Best Friend,Business Partner,Ride Or Die And A Shoulder To Always Cry On. Asante Kwa Kunionyesha Maana Halisi Ya Upendo Wa Agape(KIUNGU). Baraka Zikufuate Siku Zote Za Maisha Yako.” .
Lulu hajawahi kuposti kitu chochote kile mtandaoni tangu mwaka jana ahukumiwe jela na baadae kutolewa jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ujumbe huo pia ameutoa leo ikiwa ni siku ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Majizzo. Mashabiki wake wameoneshwa kufurahishwa zaidi na kitendo hicho kwa kuishambulia posti hiyo kwa kumkaribisha mitandaoni.
NancyTheDreamtz Huu kwa mujibu wa utafiti wa kabila zilizotoa wasomi wengi nchini tanzania. 1.wahaya wanapatikana mkoani kagera wakitokea bukoba na sehemu zingine za mkoa huoo 2.wagitaa wanapatikana wilaya ukerewe na musoma mjini na vijini mkoani mara 3.wachaga mkoani kilimanjaro wa wilaya ya moshi mjini,marangu,hai na sehemu zingine 4.wanyakyusaa mkoani mbeya wapo haswa wilaya ya kyela,songwe na zinginezo. 5.wakurya mkoani mara wilaya ya tarime na serengeti 6.wajaluo mkoani mara wilaya ya rorya na serengeti pia 7.wangoni wanatokea mkoa wa ruvuma 8.wapare wanatokea mkoa kilimanjaro wilaya ya same. 9.wasukuma hawa wapo mwanza na shinyanga 10.wanyamwezi hawa wanatokea mkoani tabora
NancyTheDreamtz Jeshi la Uganda limezindua mifuko ya kondomu katika kambi yake ya kijeshi ya UPDF Bombo iliyopewa kibwagizo cha usiende nyama kwa nyama. Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Brigedia Leopoldo Kyanda amesema mwanajeshi hawezi kutekeleza wajibu wake ipasavyo bila wenyewe kujilinda kutokana na maambukizi ya zinaa na hususan virusi vya ukimwi. Kondomu hizo zimepewa jina Ulinzi na zinatarajiwa kusaidia katika juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vinavyosababisha Ukimwi. Kitengo cha kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi jeshini kilizindua nembo hiyo mpya kwa ushirikiano na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali.
Comments