Drake na Meek Mill wamaliza bifu lao mbele ya mashabiki

NancyTheDreamtz

Baada ya ma-rapper wawili nchini Marekani Meek Mill na Drake mwaka 2015 kuingia kwenye bifu zito la kutupiana maneno makali, hatimaye wawili hao kwa sasa wamemaliza bifu lao.

Wawili hao wameuthibitishia umma jana usiku mjini Boston nchini Marekani  kwenye jukwaa la tamasha la Aubrey and the Three Migos, ambapo Drake alipanda  na kutumbuiza na Drake kisha kukumbatiana na kuonesha ishara kuwa wawili hao kwa sasa ni marafiki.

Meek Mill alipanda jukwaani na kuungana na Drake kisha kuanza kutumbuiza wimbo wa Dreams and Nightmares pamoja huku mamia ya watu wakipiga makelele ya furaha.

Drake na Meek Mill waliingia kwenye bifu kali baada ya mrembo Nicki Minaj kuingia kwenye mahusiano na Meek Mill na kuanza kumtumia vijembe Drake jambo ambalo liliamsha hisia kali kwa Drake na kumjibu Meek Mill kwa wimbo wa Back to Back. Tazama video ya wawili hao wakitumbuiza jana jukwaani

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele