Rais Magufuli apingana na Waziri wake wa Afya, asema Watanzania zaeni hakuna uzazi wa mpango

NancyTheDreamtz
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepingana na sera ya serikali yake ya uzazi wa mpango akidai kuwa sera hiyo inapunguza nguvu kazi kwa taifa.
Image result for Rais Magufuli
Rais Magufuli
Rais Magufuli akiwahutubia mamia ya watu leo Septemba 9, 2018 mjini Meatu Mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa, amesemW watanzania waendelee kuzaa lakini wachape kazi ili kukidhi mahitaji ya watoto wao.
Najua Waziri wa Afya Ummy Mwalimu hapa angependa kuongelea mambo ya uzazi wa mpango lakini mimi mengine huwa sikubaliani nayo sana, utapangiwaje kuzaa ?..Kwahiyo katika kushauriwa mengine tukubali na mengine tukatae tutumie msemo wa mzee Jakaya Kikwete ‘Ukiwambiwa changanya na za kwako’ kuzaa ni muhimu’”amehoji Rais Magufuli na kutolea mfano wa nchi ambazo alishawahi kuishi na hakusikia wimbo wa uzazi wa mpango.
Mimi Ulaya nimekaa, nafahamu madhara ya kutokuzaa, nchi gani sijaenda, Japan nimekaa, Uingereza nimekaa mwaka mzima, Ujerumani nimekaa, Canada nimekaa na nikachaguliwa kuwa co-chair wa mawaziri ardhi duniani, Denmark, Norway, utanidanganya wapi, China nimefika,“amemaliza Rais Magufuli.
Mwaka huu Serikali kupitia Wizara ya Afya, inayoongozwa na Mhe. Ummy Mwalimu imetenga Tsh Bilioni 14 kwa ajili ya huduma ya uzazi wa mpango.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele