Ommy Dimpoz atoka Afrika Kusini kwenye matibabu na kutua Kenya akiwa mwenye afya njema, abadilisha muonekano (+picha)
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
-
NancyTheDreamtz
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ambaye kwa miezi miwili amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya koromeo, hatimaye msanii huyo amepona kabisa kwa ushahidi wa picha alizopiga akiwa nchini Kenya.
Ommy Dimpoz
Kwa mujibu wa kinyozi maarufu nchini Kenya, George Dufanda ameposti picha za msanii huyo akiwa katika muonekano tofauti kabisa lakini mwenye uso wa tabasamu.
Maelezo kutoka kwa watu wanaofanya kazi karibu na Ommy Dimpoz wamesema msanii huyo amewasili nchini Kenya wiki moja iliyopita ma ameahidi kufanya Birthday Party yake nchini humo Septemba 17.
Bado haijajulikana kwa nini Ommy Dimpoz hajafikia Tanzania nyumbani kwake moja kwa moja. Tazama picha zake akiwa na kinyozi huyo maarufu nchini Kenya.
Ommy Dimpoz akiwa na kinyozi aliyemnyoa
Ommy Dimpoz wiki mbili zilizopita alirudishwa tena nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania kwa kutazamwa maendeleo ya afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa koromeo miezi miwili iliyopita.
NancyTheDreamtz Huu kwa mujibu wa utafiti wa kabila zilizotoa wasomi wengi nchini tanzania. 1.wahaya wanapatikana mkoani kagera wakitokea bukoba na sehemu zingine za mkoa huoo 2.wagitaa wanapatikana wilaya ukerewe na musoma mjini na vijini mkoani mara 3.wachaga mkoani kilimanjaro wa wilaya ya moshi mjini,marangu,hai na sehemu zingine 4.wanyakyusaa mkoani mbeya wapo haswa wilaya ya kyela,songwe na zinginezo. 5.wakurya mkoani mara wilaya ya tarime na serengeti 6.wajaluo mkoani mara wilaya ya rorya na serengeti pia 7.wangoni wanatokea mkoa wa ruvuma 8.wapare wanatokea mkoa kilimanjaro wilaya ya same. 9.wasukuma hawa wapo mwanza na shinyanga 10.wanyamwezi hawa wanatokea mkoani tabora
MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva, Benham Paul ‘Ben Pol’, usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2021 amefanya shoo ya aina yake jijini Mwanza kwenye tamasha lake la Nandy Festival 2021. Nandy, amesindikizwa na wanamuziki wengine akiwemo Baba Levo, Fid Q, Meja Kunta na wengine. NancyTheDreamtz
NancyTheDreamtz Na Mwandishi Wetu, MOHA, Songea. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amemuondoa madarakani Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Ruvuma, Seif Mgonja kwa kosa la kutogawa kwa wananchi Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN), 14,493 tangu Disemba 31, 2019, licha ya kuzalishwa na Makao Makuu na kuletewa ofisini kwake Mjini Songea. Pia Waziri Lugola amemuondoa madarakani Afisa wa NIDA Wilaya ya Namtumbo, Mkoani humo, Thobias Nangalaba kwa uzembe wa kutofika katika kikao chake cha viongozi wa Mkoa na Wilaya, licha ya kupewa taarifa ya kuhudhuria kikao hicho. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Soko Kuu la Manispaa ya Songea Mkoani humo, leo, Waziri Lugola amesema, amewatengua vyeo maafisa wawili hao kwa kucheza na kazi za Serikali, kwa kutojali majukumu yao. “Ndugu wananchi wa Songea, maafisa hawa wamekuwa wakienda kinyume na maagizo ya Serikali la kuwataka waweze kuwakamilishia wananc...
Comments